Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Yakubu Awapa Nondo za Utekelezaji wa Majukumu Maafisa Utamaduni na Michezo
Aug 28, 2023
Katibu Mkuu Yakubu Awapa Nondo za Utekelezaji wa Majukumu Maafisa Utamaduni na Michezo
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo leo Agosti 27, 2023 mkoani Njombe
Na Shamimu Nyaki

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu amefungua kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo leo Agosti 27, 2023 mkoani Njombe ambapo ametoa maagizo manne makubwa kwa maafisa hao ikiwemo kuongeza ushiriki wa jamii katika michezo na kuibua vipaji  vya Utamaduni, Sanaa na michezo katika maeneo yao.

Amewaagiza maafisa hao, kuandaa mikakati itakayosaidia vijana kutumia majukwaa mbalimbali kuonesha vipaji vyao pamoja na kuandaa mkakati wa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili ambao umeanza kujitokeza katika jamii.

"Serikali inaendelea kuongeza wataalamu wa michezo kupitia Chuo Cha Michezo Malya ambacho sasa kinafanyiwa maboresho makubwa ikiwemo ujenzi wa hosteli mpya ambayo itasaidia ongezeko la udahili wa wanafunzi chuoni hapo", amesema Katibu Mkuu Yakubu.

Baadhi ya Maafisa Utamaduni na Michezo walioshiriki kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo leo Agosti 27, 2023 mkoani Njombe


Bw. Yakubu ametoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha Kitengo cha Utamaduni na Michezo kinatengewa bajeti ya kutosha ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Katibu Mkuu Yakubu ametumia nafasi hiyo kugawa vifaa vya michezo ikiwemo mipira  54 ya mchezo wa Mpira wa Miguu, Kikapu na Wavu ambayo itagawiwa kwa mikoa yote nchini kwa ajili ya mashindano ya Samia Cup yanayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi