Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Mhandisi Mtigumwe Amtembelea Msindikaji wa Nafaka Busega
Jun 18, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Juni, 17 2019 akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu amepata fursa ya kumtembelea muwekezaji mzawa wa kusindika nafaka Bw. Deogratius Kumalija katika Wilaya ya Busega.
Akiwa kiwandani hapo Mhandisi Mtigumwe alipata maelezo kutoka kwa mmiliki huyo kuwa ameamua kujikita katika usindikaji wa mazao ya nafaka kutokana na fursa iliyopo katika kuongeza thamani ya mazao hayo hususani mahindi na mpunga.
Bw. Kumalija aliendelea kusema kuwa kiwanda hicho cha mpunga kina uwezo wa kukoboa Tani 28 kwa siku na alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kupanga madaraja ambapo kiwanda cha kusaga Mahindi kipo katika ujenzi na punde kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusaga tani zaidi ya 30 za mahindi kwa siku.
Alisema kuwa viwanda hivyo vitasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo na kuondokana na nchi kuendelea kuuza mazao ghafi.
Kadhalika, Mhandisi Mtigumwe alimpongeza muwekezaji huyo kuwa aendelee na uwekezaji huo pia Serikali imekuwa ikisisitiza kuyaongezea thamani mazao ya Kilimo.
Hivyo mwekezaji kama Bw Kumalija anatimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozw ana mHe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Sera ya Viwanda.
Hata hivyo kwa kuwa na Viwanda kama hivyo vitaongeza ajira na kuhamasisha wakulima kulima wakiwa na uhakika wa mazao yao na kuyaongezea thamani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi