[caption id="attachment_41657" align="aligncenter" width="1000"]
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza na wafanyakazi wa Wizara yake Aprili 02, 2019 Jijini Dodoma kuhusu kuboresha utendaji kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.[/caption]
Na Shamimu Nyaki -WHUSM
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi amesema kuwa ujenzi wa Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma zipo katika hatua za mwisho kukamilika na kuwataka watumishi wake kuwa tayari kuhamia kati ya mwezi wa nne na wa tano mwaka 2019.
Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma wakati wa kikao na Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilicho wapa fursa wafanyakazi hao kiliwakutanisha fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali ya kiutendaji.
“Ni vyema mkajiandaa na kuwa tayari kuhamia mji wa Serikali kwakua kwa sasa ofisi zipo katika hatua za mwisho kukamilika na matarijio yangu ni kwamba kati ya mwezi wanne na wa tano tutakuwa tumehamia rasmi”.alisema Bibi.Susan.
[caption id="attachment_41654" align="aligncenter" width="1000"]Aliongeza kwa kueleza kuwa Wizara imefanya michakato mbalimbali ya kuhakikisha inawakwamua watumishi wake kiuchumi kwa kuanzisha SACCOS pamoja na Mfuko wa kufarijiana wenye lengo la kuwasaidia watumishi katika masuala mbalimbali ya kijamii .
Aidha Katibu Mkuu huyo amewataka watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo ili kuleta matokeo chanya katika utendaji, huku akisisitiza kuwa hakuna haki bila wajibu.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Orest Mushi amewataka watumishi hao kufuata na kuzingatia sheria , taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma katika utendaji wa kazi.
[caption id="attachment_41656" align="aligncenter" width="1000"]