Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi Aipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu Usimamizi Mzuri wa Ujenzi wa Mji wa Serikali
Oct 05, 2023
Katibu Mkuu Kiongozi Aipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu Usimamizi Mzuri wa Ujenzi wa Mji wa Serikali
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka akizungumza wakati wa ziara ya Makatibu Wakuu katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu - Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Uratibu na Usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Ametoa pongezi hizo mapema leo, tarehe 5 Oktoba 2023 alipokuwa katika ziara maalum ya Makatibu Wakuu ya kutembelea mji wa Serikali Mtumba Dodoma ambapo alisema mafanikio ya mradi huu wa ujenzi wa Mji wa Serikali ni kukamilika kwa ukamilifu wake akitolea mfano ujenzi wa Uwanja wa Mashujaa kuwa ni alama kubwa ambao utatumika kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na wageni kujifunza nini ambacho Tanzania imefanya.

“Tunathamini kazi yenu kubwa sana mnayofanya, kama tulivyosema awali kwenye Wasilisho, hii kazi inahitaji Uratibu kwa Sababu ni kazi ya Serikali, siyo kazi ya mmoja kuwa amemaliza na wengine kujisikia vibaya, tunashukuru kwa kutupitisha kwenye kazi kuanzia mwanzo, tumeona juhudi kubwa za wataalamu wetu na wasimamizi lakini pia tumeona kazi kubwa iliyopo mbele na tunatambua kwamba baadhi ya wadau wanakaribia kumaliza kazi zao.” Alisema Mhe. Balozi Kusiluka.

 Aliendelea kusema kuwa bado kuna muda wa kutosha wa kutatua changamoto ndogo zilizobainika katika ziara hiyo na kusisitiza kuutazama mradi huo kwa ujumla wake kama Serikali moja, na kazi ya uratibu ikiendelea lakini pamoja na kuimarisha timu ya wataalamu wa ngazi zote katika ujenzi na kuwasikiliza, “Ni fursa pekee ambayo tumepewa ya kujenga Makao Makuu ya Serikali mapya na Serikali imetoa fedha nyingi kwa hivyo ni lazima sisi wataalam tufanye kazi inavyopaswa.” Alisisitiza.

Alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo, na kuwapa uhuru wataalam kufanya kazi ya kitaalam inavyopaswa, na kushauri wadau wengi kushiriki katika kazi hiyo pamoja na kujadili mambo ya kitaalam ili watu wengi waweze kujifunza

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonaz alisema swala la ushirikishwaji wa wataalam katika ujenzi wa mji wa Serikali ni swala la muhimu sana, na wadau mbalimbali wanashirikishwa kwa ajili ya kuja kuwekeza katika maeneo mbali mbali ambayo yametengwa katika mji huo wa Serikali,na majengo hayo ya Mji wa Serikali yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi