Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Karibu Dodoma Festival Lapiga Hodi
Aug 12, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Adeladius Makwega, WHUSM-Dodoma

Wasanii mkoani Dodoma wameandaa tamasha linalofahamika kama Karibu Dodoma litakalofanyika Oktoba 2021 ambalo lengo lake ni kutangaza miradi kadhaa ya kimkakati na ile isiyo kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Tano na Sita.

Wakizungumza katika kikao cha pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Mji wa Serikali-Mtumba Jijini Dodoma, kamati ya maandalizi imesema kuwa tamasha hilo litakuwa la kukata na shoka kwani litabeba kazi zote za Serikali ambapo miradi yote inyogusa jamii itaoneshwa.

“Tumejiandaa vilivyo na tunawajulisha Watanzania wote kuja kushuhudia tamasha hili ambapo Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo tumeiomba taasisi zake kama BASATA, COSOTA ziwepo ili kuweza kutoa huduma mbalimbali kwa watakaokuja kutazama tamasha letu.”, alisema Saimon Mwapagata ambaye ni msanii wa filamu nchini, akiwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo.

Tamasha hili litawakutanisha wasanii mbalimbali kama vile wa ngoma za asili, muziki wa kizazi kipya, filamu na vichekesho.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mfaume Said amesema kuwa wamefanya kikao  na kamti hiyo kwa pamoja wamekubaliana kuanza maandalizi ya kina kukamilisha tamasha la karibu Dodoma.

“Jambo hili ni la sekta yetu, tumelipokea, tumelijadili na tumekubaliana lifanyike Oktoba 2021 katika viwanja vya Nyerere Square.”Alisema Bw, Said

Mwenyekiti huyo wa kamati ya maandalizi aliambatana na katibu wake, Eusted Rwegoshora na mjumbe Bi. Wema Sekamba.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi