[caption id="attachment_7516" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa tamasha la Chemichemi Carnival Bi. Lena Kimani akisisitiza juu ya tamasha litakalofanyika tarehe 9 na 10 mwezi Septemba 2017 katika kijiji cha Makumbusho wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Zechy Africa, Bi. Dorah Raymond na Mkurugenzi wa Operesheni wa Kampuni ya Zechy Africa Bw. Ally Nchahaga (kushoto).[/caption]
Na. Thobias Robert
Kampuni ya Zechy Africa inayojihusisha na masoko imeandaa tamasha kwa ajili ya kusherehekea utamaduni wa Mtanzania linalotarajiwa kufanyika mapema mwanzoni mwa mwezi wa tisa katika Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa tamasha hilo Bi. Lena Kimani alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Tamasha hilo linaloitwa Chemichemi Carnival na kusisitiza kuwa tamasha hilo litafanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 9 -10 mwaka huu.
[caption id="attachment_7519" align="aligncenter" width="640"]Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Dorah Raymond amesema kuwa Tamasha hilo linatarajia kuwakutanisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi ili kukuza fursa ya kiuchumi kupitia sanaa na tamaduni zitakazooneshwa katika tamasha hilo.
Alisema kuwa tamasha la hilo linaleta watu wote pamoja katika kusherehekea tamaduni zetu lakini pia fursa za kukua kiuchumi kupitia sanaa.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Zechy Africa Bw. Ally Nchahaga ameongeza kuwa kufuatia umuhimu wa kukuza utamaduni wa mtanzania tamasha la Chemichemi Carnival litakuwa likifanyika mara mbili kwa mwaka.
“Tamasha hilo ambalo litafayika kwa mara ya kwanza hapa nchini, halitakuwa na kiingilio, badala yake wananchi wahamasishwa kujitokeza kwa wingi wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ili kuongeza hamasa,” aliongeza Ally Nchahaga
Kampuni ya Zechy Africa imeandaa Tamasha hilo ikiwa ni mara ya kwanza kwa tamasha hilo kufanyika hapa nchini ambapo kupitia kampuni hiyo litakuwa likifanyika kila baada ya miezi sita ili kutoa fursa kwa tamaduni mbalimbali kushiriki katika tamasha hilo.