Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kamishna Uhamiaji Zanzibar afanya ziara Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja
Nov 23, 2017
Na Msemaji Mkuu

Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kusini Mkaguzi Msaidizi  wa Uhamiaji, Kheri Shabani akitoa mkono wa salamu kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipowasili kwenye Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo,   tarehe 21 - 22 Novemba, 2017. 
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akitia saini kitabu cha wageni, mara tu alipowasili Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani humo, Leo tarehe 22 Novemba, 2017. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mkemimi Mohamed Mhina.
 
 Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Khamis Ali Juma akitoa maoni juu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika eneo la uendeshaji wa mashtaka ya Kiuhamiaji, wakati wa kikao cha pamoja cha Wafanyakazi wa Mkoa wa Kusini Unguja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, Akijibu hoja mbali mbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo, tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.  Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdullah Mbarouk Ramsa.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akielezea jinsi Idara ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika kutatua changamoto ya Makaazi ya Askari wake katika Wilaya zote Unguja na Pemba. Aliayasema hayo wakati akikagua nyumba za Watumishi wa Uhamiaji iliyopo Makunduchi, Wilaya ya Kusini, wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika tarehe 21 - 22 Novemba, 2017.Imetolewa Na: Kitengo Cha Uhusiano, Ofisi Kuu Ya Uhamiaji Zanzibar  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi