Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JPM Awataka Wafanyabiashara Kuwekeza Katika Viwanda Vya Madawa
Nov 25, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23388" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila mapema hii leo.[/caption]

Na: Jonas Kamaleki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara kuweza katika viwanda vya madawa ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa bidhaa hiyo nchini.

Rais Magufuli ameto wito huo leo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wakati akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Syansi Shirikishi Muhimbili.

“Wafanyabiashara tumieni fursa hii ili muweze kuwekeza katika viwanda vya madawa kwani Tanzania imepewa nafasi ya kuuza dawa katika nchi za SADC na tumetenga zaidi ya bilioni miambili kwa ajili ya kununulia madawa,”amesema Rais Magufuli.

[caption id="attachment_23389" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mloganzila wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila mapema hii leo.[/caption]

Ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kujenga kiwanda cha madawa Mloganzila badala ya kukkopesha fedha hizo kwa watu wanaojenga nmajumba.

Magufuli amesema kuwa Serikali imedhamira kuwekeza katika masuala ya Afya ili kuwa na Taifa lenye watu wenye afya ili wawezekushiriki katika ujenzi wa viwanda. Bila afya njema hakuna ambacho kitafanyika, alisisitiza Rais Magufuli.

Katika Chuo kitakachojengwa Mloganzila kikitumika apmoja na hospitali hiyo, Rais Magufuli amesema kitatola wataalaam wenye ubora ambao utaendana na hadhi ya chuo hicho.

Ili kuongeza ufanisi katika hospitali za mikoa, Rais ameshauri zisimamiwe na wizara ya afya kuliko ilivyo sasa ambapo zilikuwa zikisimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

“Hospitali hizo haziwezikusimamiwa na watu ambao sio wataalaamu wa tiba, hivyo hospitali zote za mikoa ziwe chini ya wizara ya Afya ambayo ndiyo inasimamia Sera ya Afya, na hizo nyingine za wilaya, kata na vijiji ndizo zisimamiwe na TAMISEMI, alisema Rais Magufuli.

Amesema kwa usimamizi huo sekta ya Afya itaimarika kuanzia ngazi ya mikoa hadi Taifa.

Rais Magufuli amewataka madaktari na wahudu wa afya hapo katika Hospitali ya Mloganzila kutunza vifaa na miundombinu ya hospitali hiyo ili kuhakikisha ubora uliopo sasa hivi uweze kudumu.

Amewataka kutoharibu vifaa hivyo vya kisasa ambavyo Rais amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na ina hadhi kama hospitali za Ulaya.

Kwa upande wa Bima za Afya, Rais magufuli amewataka wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ambayo itawahakikishia upatikanaji wa matibabu.

“Msiendekeze ununuzi wa nguo, starehe bali changieni katika mifuko hiyo ambayo itawasaidia watoto wenu kupata matibabu ya uhakika, ukiuza majogoo wawili utaweza kumlipia mwanao gharama za matibabu kwa mwaka,”alisisitiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais amewataka mawaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana katika kuendesha hospitali za Muhimbili na Mloganzila.

Amewambia kuwa umimi hauhitajiki katika masuala ya kitaifa hivyo wizara hizo zishirikiane katika kuhakikisha ufanisi wa Hospitali ya Mloganzila.

Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Apolinary Kamuhabwa amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za tiba ya dhararula kwa watu wazima na watoto, huduma za magonjwa ya akina mama na mfumo wa uzazi, magonjwa ya macho, mfumo wa pua, koo na masikio na magonjwa ya akili.

Kwa mujibu wa Prof. Kamuhabwa huduma nyingine zitakazotolewa na hospitali hiyo ni pamoja na hmatibabu ya magonjwa ya mifupa na majeruhi, upasuaji mkubwa na mdogo, huduma za kusafisha damu kwa magonjwa ya figo na tiba za magonjwa mbalimbali zikiwemo za kinywa.

Hospitali ya Mloganzila imejengwa na Serikali ya Tanzania na Korea ya Kusini ambayo imetoa mkopo wa masharti nafuu. Ujenzi wa Hospitali umegharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 94.5 (USD) ambapo Serikali ya Tanzania imetoa jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.4.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi