Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKT Yasitisha Mafunzo kwa Kundi la Kujitolea
Jan 19, 2021
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha kwa muda Mafunzo kwa kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 kwa vijana waliokuwa wamechaguliwa  kushiriki mafunzo hayo yaliyotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini kote.

Hayo yamesemwa  leo  na Kaimu  Mkuu wa Utawala, Kanali Hassan Mabena wakati wa mkutano wake  na waandishi wa habari uliofanyika  Makao Makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

“Kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujitolea warejee majumbani kwao” alisisitiza Kanali Mabena.

Pamoja na hayo, Kanali Mabena amewataka vijana ambao walikuwa hahawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka watakapotangaziwa tena.

Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiwajengea vijana uwezo wa kujiajiri kupitia stadi za maisha wanazopata katika mafunzo yanayotolewa kwa mujibu wa sheria na yale ya vijana kujitolea, hivyo kuwawezesha kuwa wazalendo wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi waTaifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi