Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imefanikiwa kutoa huduma kwa nchi za Afrika zenye uhitaji wa matibabu ya moyo kwa wananchi wake.
Akieleza mafanikio ya Taasisi hiyo leo Februari 26, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Peter Kisenge amesema wataalamu wa Taasisi hiyo walivuka mipaka ya nchi na kwenda kutoa huduma za matibabu ya moyo katika nchi za Malawi, Zambia, na Jamhuri ya Watu wa Comoro.
"Katika nchi hizo walitibiwa wagonjwa 1,189 kati yao, watu wazima walikuwa 851 na watoto 338, wagonjwa 262 walipewa rufaa ya kuja kutibiwa JKCI ", alisisitiza Dkt. Kisenge
Aidha, Dkt. Kisenge amebainisha kuwa wagonjwa waliotoka nje ya nchi kuja JKCI kupata huduma za matibabu walikuwa 689 na walitoka katika nchi za Somalia, Malawi, Kenya, Rwanda, Msumbiji, Nigeria, Siera Leone, Zimbambwe, Zambia, Uganda, Congo, Ethiopia, Burundi, Arnemia, China, India, Ujerumani, India,Norway, Ufaransa na Uingereza.