Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Mbioni Kuanzisha Ushirikiano wa Utoaji Huduma za Matibabu ya Moyo na Hospitali ya Ostrava
Feb 11, 2022
Na Jacquiline Mrisho


Na: Mwandishi Maalum

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iko mbioni kuanzisha ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri ya Watu wa Czech.

Akizungumza baada ya kufanya ziara JKCI leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa msafara wa madaktari sita kutoka nchini Czech Miroslav Homza amesema kuwa lengo kubwa la madaktari hao kufika JKCI ni pamoja na kuangalia jinsi ambavyo wataweza kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo ikiwa ni njia yakubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Czech.

“Tumefika hapa JKCI na kukutana na uongozi kujadilina juu ya uwezekano wa madaktari kutoka JKCI na wale wa Hospitali ya Ostrava iliyopo Jamhuri wa watu wa Czech kuweza kubadilishana uzoefu katika kutoa huduma zamatibabu ya moyo haswa upande wa upasuaji wa moyo”,

“Sambamba na kutoa huduma za matibabu ya moyo, pia tutaangalia namna gani tunaweza kushirikiana upande wa utafiti katika masuala ya magonjwa ya moyo kati yetu naTanzania”, alisema Homza.

Aidha, Homza amesema kuwa katika ushirikiano huo Czech itaangalia kama kuna uwezekano wa wagonjwa ambao wapo Tanzania na wanahitaji huduma za matibabu ya kina kuchukuliwa na kupelekwa Jamhuri ya watu waCzech kwa ajili ya matibabu hayo kwani Czech inatoa huduma za matibabu ya hali ya juu na kwa gharama nafuu tofauti na nchi nyingine duniani.

Akizungumzia ushirikiano wa kutoa huduma za matibabu ya moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa JKCI imekua ikishirikiana na madaktari kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuongeza uzoefu na kutoa huduma bora na za kibingwa za matibabu ya moyo.

“Leo tumepokea madaktari kutoka Jamhuri ya watu wa Czech ambao wamefika kujadiliana nasi namna ambavyo tutashirikiana katika kubadilishana uzoefu wa kutoa huduma za matibabu ya moyo, tumekubaliana kuandaa mkataba wa makubaliano ambao utatuongoza katika kushirikiana na kusaidia katika kubadilishana uzoefu huo”, alisema Prof. Janabi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi