Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jamii Yatakiwa Kuyatunza Mazingira Kulinda Ardhioevu.
Feb 04, 2021
Na Msemaji Mkuu

Tanzania ni moja wapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa ardhioevu na viumbe mbalimbali vinavyoishi kwa kutegemea utajiri huo,  hivyo jamii imetakiwa kuyatunza mazingira ili kuulinda utajiri huu adhimu na adimu.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho, Dkt. Gwakisa Kamatula kwenye maadhimisho ya wiki ya ardhioevu duniani yaliyofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais nchini.

Akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga, Dkt. Gwakisa amesema kuwa baadhi ya ardhioevu nchini zimekuwa zikiharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za binadamu zikiwemo kilimo, ukataji miti ovyo, uchafuzi wa maji na ardhi, matumizi mabaya na yasiyoendelevu ya maji, ufugaji usioratibiwa na mengineyo mengi.

“Hali hii inasababisha kupungua kwa maji na ubora wake, kupungua kwa mazalia ya samaki na wanyamapori, kupungua kwa mazao ya chakula, na ukame wa muda mrefu”. Aliongeza Dkt Kamatula.

Mhifadhi Mwadamizi wa Baolojia kutoka Makubusho ya Taifa, bibi Adelaide Salema amesema Programu hiyo imejumuisha onesho, kutembelea baadhi ya ardhioevu kupata uelewa halisia, onesho la video ”virtual exhibition/digital form” na onesho dogo katika moja ya kumbi za maonesho za Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

“Programu ya maadhimisho kwa mwaka huu imelenga kuelimisha umma, kujua athari zinazosababishwa na matumizi yasiyo endelevu kwenye ardhioevu na namna ya kukabiliana na athari hizo. Walengwa wakuu ni wanafunzi na jamii kwa jumla”. Alisema Bibi Salema

Akizungumzia umuhimu wa ardhioevu, Mhifadhi Mwandamizi wa Baolojia wa Kijiji cha Makumbusho, Bibi Agnes Robart amesema kuwa ardhioevu ina umuhimu na faida kubwa si tu kwa wanyamapori na mimea bali kwa mwanadamu ambaye shughuli zake za kila siku anategemea maji.

Kutokana na umuhimu huu Makumbusho ya Taifa imeandaa programu maalumu ya kujivunia urithi wa asili ambao unapatikana kwenye ardhioevu

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi