Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jamii Yatakiwa Kuwa na Utamaduni wa Kusoma Vitabu
Jun 26, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53599" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu akizungumza kwa niaba ya Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Wizara hiyo katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoitwa “Rais Magufuli na Serikali yake walivyobomoa Hekalu na kulijenga upya”kilichoandikwa na Mwl. Projestus Vedasto Kabagambe uliofanyika jana Jijini Dodoma.[/caption]

Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dodoma

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu ametoa wito kwa Watanzania kuwa na Utamaduni wa kusoma vitabu ili kuongeza ujuzi na maaarifa pamoja na kuijua historia ya taifa.

Dkt. Temu ameyasema hayo jana Jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe kinachoitwa “Rais Magufuli na Serikali yake walivyobomoa Hekalu na kulijenga upya” kilichoandikwa na Mwl. Projestus Vedasto Kabagambe wa Shule ya Sekondari Viwandani, Dodoma ambapo amesema kwamba utamaduni wa kusoma vitabu unasaidia kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali ikiwemo uwajibikaji kwa nchi, uzalendo wa kulinda rasilimali za nchi pamoja na kujituma.

[caption id="attachment_53600" align="aligncenter" width="1000"] Mwl. Projestus Vedasto Kabagambe wa shule ya Sekondari Viwandani iliyopo Dodoma ambaye ni mwandishi wa kitabu kinachoitwa “Rais Magufuli na Serikali yake walivyobomoa Hekalu na kulijenga upya”, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanywa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu  kwa niaba ya Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Wizara hiyo uliofanyika jana Jijini Dodoma.[/caption]

“Watanzania tumekuwa wazito wa kuandika na kusoma vitabu, ni vizuri tukabadilika na kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili taifa liweze kupata wataalam waliobobea katika sekta mbalimbali”, alisema Dkt. Temu.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano umeonekana ikiwemo kutoa elimu bila malipo mashuleni, ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, kujenga ukuta wa Mirerani na mengine mengi ambapo  Mwandishi ameamua kuhifadhi utekelezaji huo katika maandishi ili vizazi na vizazi vije kusoma na kuenzi utumishi huo.

[caption id="attachment_53598" align="aligncenter" width="848"] Dkt. Elizabeth Msoka kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John’s cha Dodoma akitoa maoni kuhusu kitabu kilichoandikwa na Mwl. Projestus Vedasto Kabagambe wa shule ya Sekondari Viwandani iliyopo Dodoma kinachoitwa “Rais Magufuli na Serikali yake walivyobomoa Hekalu na kulijenga upya”, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanywa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu  kwa niaba ya Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Wizara hiyo uliofanyika jana Jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake Mwalimu Projestus Vedasto Kabagambe, Mwandishi wa Kitabu hicho amesema kuwa lengo la kitabu ni kueleza utekelezaji wa kasi uliofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake wa kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia miradi ya kimkakati ambayo ilishindwa kutekelezwa kwa miaka mingi tangu kuasisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere.

“Kitabu hiki kina lengo la kuieleza jamii umuhimu wa kuwajibika, lakini pia kuhamasisha jamii kuiga mfano wa Rais wetu ambaye ni mzalendo wa kweli kwa nchi yake kwa namna ambavyo amefanya makubwa katika nchi hii kwa kipindi kifupi cha uongozi wake”, alisema Mwl. Vedasto.

[caption id="attachment_53597" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu akizindua kitabu kilichoandikwa na Mwl. Projestus Vedasto Kabagambe wa shule ya Sekondari Viwandani kinachoitwa “Rais Magufuli na Serikali yake walivyobomoa Hekalu na kulijenga upya”, kwa niaba ya Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Wizara hiyo uliofanyika jana Jijini Dodoma.[/caption]

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha ST. John’s Dodoma ambaye ni miongoni mwa wahariri wa kitabu hicho amesema kuwa kitabu hicho chenye Sura kumi na tatu kimeleeza kwa kina dhana ya uwajibikaji wa viongozi pamoja na wanajamii katika maeneo yote ambayo ndio falsafa ya uzalendo ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi mbalimbali wanazotoa kwa wananchi kama alivyotekeleza Dkt. Magufuli Rais wa Tanzania.

Dkt. Elizabeth ameongeza kuwa maudhui ya kitabu yatasaidia jamii kuelewa umuhimu wa kuwa wazalendo kwa kila jambo pamoja na kuamini katika dhana ya kujitambua na kujitegemea kwa kufanya rejea ya yale yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi