Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jaji Mkuu Afungua Kikao cha Wadau Kujadili Kazi ya Ulinganisho wa IJA
Apr 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30480" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso akiongea jambo na Wadau walioshiriki katika kikao hicho, katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.[/caption] [caption id="attachment_30481" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, alipokuwa akielezea kuhusu Chuo hicho.[/caption] [caption id="attachment_30482" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe wa Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo cha Kodi n.k, Washiriki wakifuatilia kwa makini, katika kikao hicho Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania wamechukua maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao na wameahidi kuyafanyia kazi katika kuboresha Mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho kwa manufaa ya Watumishi wa Mahakama na Wananchi kwa ujumla.[/caption] [caption id="attachment_30483" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wajumbe wa Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo cha Kodi n.k, aliyeketi nyuma wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila.[/caption] [caption id="attachment_30484" align="aligncenter" width="750"] Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akifungua Kikao cha Wadau Kujadili kazi ya ulinganisho wa chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) na Vyuo vingine vya Mafunzo endelevu. Kikao hicho kati ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama na Wadau wa Vyuo vingine vinavyotoa mafunzo endelevu kimelenga katika kujadili uzoefu na nafasi ya ushirikiano wa karibu baina ya Chuo hicho na Vyuo vingine vya Umma vinavyotoa mafunzo endelevu kwa Watumishi wa umma na Wadau mbalimbali katika Sekta ya Sheria, kikao hicho kilifanyika Aprili 16 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_30485" align="aligncenter" width="750"] Picha ya pamoja ya ushiriki: aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso, wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila, wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali na wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA).
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi