Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jafo Mgeni Rasmi Kongamano la Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
Dec 04, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24067" align="aligncenter" width="750"] Wajibu 1: Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU –Institute of ublic Accountability Ludovick Utouh (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Kongamano la siku mbili la Uwajibikaji kwa Mamlaka za Serikali za Mtaa linalotarajiwa kuanza kesho Jijini Dar es Saalam, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus na kushoto ni Afisa Tafiti wa Taasisi hiyo Hassan Kisena.(Picha na Eliphace Marwa)[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamono la siku mbili litakaloanza tarehe 5-6 Desemba mwaka huu na kujadili ushiriki na uwajibikaji wa mamlaka za Serikali za Mitaa katika ujenzi wa uchumi wa kati kupitia viwanda nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji kwa Umma (WIPA), Ludovick Utouh alisema kongamono hilo limekusudia kujadili  sera, miongozo na mikakati iliyowekwa na Serikali katika ujenzi wa viwanda  inavyotekelezwa katika ngazi za Halmashauri.

Utouh alisema Serikali za Mitaa zina mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kwa kuwa ndiyo chombo kilicho karibu zaidi na wananchi katika kutoa maelezo ya mgawanyo wa usimamizi na matumizi ya rasilimali za kiuchumi katika jamii ikiwemo ardhi.

“Kongamano hili linatarajia kuwahusisha Mameya na Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini, ambapo hadi sasa jumla ya washiriki 120 wamedhitisha ushiriki wao wakiwemo Mameya 50 na Wakurugenzi Watendaji 70” alisema Utouh.

Kwa mujibu wa Utouh alisema kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi hiyo kwa kushirkiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia mradi wa GFG unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo Uswisi (SDC) katika taasisi zinazojishughulisha na utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Aliongeza kuwa katika kongamano hilo jumla ya mada 7 zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa na wajumbe wa kongamano hilo ikiwemo Mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano katika utekelezaji wa sera ya viwanda, mpango wa pili wa maendeleo ya taifa 2016/17-2020/21.

Aidha Utouh alizitaja mada nyingine kuwa ni pamoja na majukumu ya halmashauri katika utekelezaji wa sera ya viwanda, umuhimu wa uwajibikaji, mifumo ya ndani na mfumo wa kupima ardhi katika halmashauri pamoja na mada nyingine mbalimbali.

Taasisi ya Wajibu ilianzishwa mwaka 2015 kwa maelngo ya kutengeneza mazingira ya kukuza uwajibikaji na utawala bora nchini ikilenga katika kuongeza thamani katika huduma inazotoa ili kusimamia uadilifu na usawa kwa wananchi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi