Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkombozi wa Wananchi
Aug 01, 2023
Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkombozi wa Wananchi
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO kuhusu utekelezaji wa Hospitali hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Na Frank Mvungi

Hospitali ya Benjamin Mkapa imejidhatiti kuwa Kitovu cha huduma za Ubingwa Kanda ya Kati ili kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya kufuata huduma hizo jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Alphonce Chandika wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika jijini Dodoma kuelezea utekelezaji wa Hospitali hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“Mosi upandikizaji figo, kwa mwaka wa fedha ulioisha jumla ya wananchi 8 wamenufaika na upandikizaji figo, wastani wa wahuduma hii ni shilingi milioni 36  ambapo kwa wanufaika 8 wametumia jumla ya Shilingi Milioni 288 wakati hawa wangeenda nje ya nchi kupata huduma hii wangetumia shilingi milioni 600 kulingana na hospitali za nje, hivyo kwa huduma hii Serikali imeokoa shilingi milioni 312,” alisisitiza Chandika.

Sanjari na hilo, Dkt. Chandika amesema huduma za matibabu ya moyo, katika huduma hizi za moyo tumeendelea kuimarika kutoka mwaka hadi mwaka uliopita tumefanya uchunguzi wa Mishipa ya Moyo kwa wagonjwa 320, Upandikizaji Betri wagonjwa 13, Watoto waliozibwa Matundu kwenye Moyo 14, Kuweka vizibua njia ya Mishipa ya Moyo (Stents) 54.

Kuhusu vipandikizi kwenye Magoti na Nyonga (Hip and total Knee Replacement) Dkt. Chandika ameeelza kuwa jumla ya wanufaika 72 wamenufaika na huduma hii. Serikali imetumia  Milioni 864 ambapo kama wangeenda kupata huduma hii nje ya nchi ingeigharimu Serikali shilingi bilioni 2 na milioni 502.

Kutokana na uwekezaji huo, Serikali imeokoa shilingi 1,638,000,000/= aidha katika matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi huduma ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu wananchi wamenufaika na huduma hii kwa Upasuaji wa Ubongo 276 na Upasuaji Uti wa mgongo 237.


Jambo la nne na kwa ukubwa ni huduma mpya iliyozinduliwa  mwaka huu  ya upandikizaji uloto (Borne Marrow Tansplant) ambayo imefanikiwa kwa manufaa makubwa kwa watoto wa nne wamepatiwa matibabu hayo na sasa wamepona kabisa.

Huduma hii inapatikana Tanzania pekee katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati na ni Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee inayotoa matibabu, gharama za matibabu ni shilingi  milioni 50 wakati matibabu haya nje ya nchi yanapatikana kwa  shilingi milioni 120 hadi shilingi milioni 135 hii ni kusema Serikali imedhamiria kuokoa pesa na kuimarisha huduma za matibabu Tanzania.

Jambo la tano la muhimu katika kiwango cha kufikia utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi ni lazima mfanye mashirikiano ya kitaifa na kimataifa, katika hili niwe wazi Serikali ya Awamu ya Sita inayoongonzwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetufungulia na kutuwekea mazingira rafiki ya kufanya mashirikiano ya kimatibabu kama ifuatavyo; Help3 Monza ya nchini Italy, DKMS Laboratory ya nchini Ujerumani, Pathology without Bordarder – nchini Italy, Shebba Medical Hospital – nchini Izrael, Childrens Heart Charity Association – nchini Kuwait,  Chuo kikuu cha Vienna&Hospitali kuu ya Vienna – nchini Austria, Hospitali ya watoto Sanjeevani – nchini India.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi