Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Halmashauri Zatakiwa Kutumia Mfumo wa PlanRep
Aug 07, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8560" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa umma kutoka mikoa ya Songwe, Iringa, Njombe na Mbeya alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inawashirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa hiyo. Kulia ni Mwakilishi wa TAMISEMI,Bw. James Mtatifikolo na Meneja Programu wa PS3 Mkoa wa Mbeya Bw. Gasper Materu.[/caption]

Na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya

Halmashauri ambazo azijafikiwa na Program ya Uimarishaji wa Sekta za Umma (PS3) zashauriwa kutenga fedha katika bajeti zao kwa ajili ya kuziwezesha kuingizwa katika mpango huo wenye tija kwa maendeleo ya taifa.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi. Mariam A. Mtunguja wakati akifungua semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya.

[caption id="attachment_8563" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Makao Makuu Dar es Salaam Dkt. Gemini Mtei akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption]

“Tumeona namna ambavyo mfumo huu umeleta mabadiliko makubwa katika maeneo ambayo Program hii ya Uboreshaji  wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) inafanya kazi ni vyema sasa mikoa mingine ikaangalia namna kwa kutenga fedha katika bajeti zao ili iweze kuingizwa katika mradi huu muhimu”, alisema Bibi. Mariam.

Aidha Katibu Tawala huyo ameipongeza PS3 kwa kuendesha mafunzo hayo ambayo kwa namna ya kipekee yanashirikisha hata zile Halmashauri ambazo hazipo katika Programu hiyo jambo linaloonyesha dhamira halisi ya kuleta mageuzi katika mifumo ya sekta za umma.

[caption id="attachment_8565" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Bw. James Mtatifikolo akifafanua jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption] [caption id="attachment_8566" align="aligncenter" width="750"] Meneja Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) mkoa wa Mbeya Bw. Gasper Materu akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption]

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma(PS3) Makao Makuu Dkt. Gemini Mtei amesema kutokana na jitihada na uhitaji wa Serikali katika kuboresha mifumo yake wameanzisha mfumo unaorahisisha mawasiliano ya kielekroniki kwa lengo la kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Aliongeza kutokana na teknolojia kubadilika Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani wanaendesha mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo watendaji wake katika kutumia kwa ufasaha Mfumo huu mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti.

[caption id="attachment_8570" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia mada wakati wa ufunguzi wa semina hiyo leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inayoendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption] [caption id="attachment_8572" align="aligncenter" width="750"] Kiongozi wa wawezeshaji Bw. Frank Makua Charles akichokoza mada wakati wa semina katika akichokoza mada wakati siku ya kwanza ya semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hii ya siku nane inaendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID)ambapo imeshirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption] [caption id="attachment_8573" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wawasilisha mada kutoka OR – TAMISEMI Bw. Jeremia Mtawa akiwasilisha mada kuhusu namna mfumo wa PlanRep utakavysaidia katika kuimarisha utendaji wa Halmashauri nchini wakati wa semina semina ya siku nane kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma katika upangaji mipango na bajeti (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hii ya siku nane inaendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inashirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption] [caption id="attachment_8574" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dar es Salaam Dkt. Gemini Mtei akiwasilisha mada kuhusu Uimarishaji wa Mfumo wa Sekta za Umma (PlanRep) utakavyosaidia katika upimaji matokeo na utendaji wa Halmashauri nchini, wakati wa semina kuhusu mfumo huo leo Jijini Mbeya. Semina hii ya siku nane inaendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID)ambapo imeshirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.[/caption] [caption id="attachment_8575" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akiagana na Meneja Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Mbeya Bw. Gasper Materu mara baada ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inahusisha watumishi wa umma kutoka kada za Maafisa Mipango, Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu kutoka Halmashauri na Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.Katikati ni Mwakilishi wa Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dar es Salaam Dkt. Gemini Mtei.[/caption]

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Bw. James Mtatifikolo amesema kuwa PlaRep ni mfumo ambao umelenga kuunganisha mifumo yote na kuwa na kanzi data moja kwa sekta zote za umma.

“Tumekuwa na mifumo mingi ambayo kimsingi imekuwa ikisababisha kuwepo kwa taarifa zinazokinzana, hivyo kupitia mfumo huu mpya matatizo yote yametatuliwa  na kuondoa mkanganyiko iliyokuwa ikijitokeza kutokana na kuwepo kwa mifumo tofautitofauti”, aliongeza Bw. Mtatifikolo.

Semina hii ni muendelezo wa mafunzo yaliyoandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na USAID kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi ya watumiaji 1,500 wa mfumo huu Tanzania nzima ambapo katika awamu ya kwanza yalihusiha mikoa ya Kanda ya ziwa na Kusini yaliyofanyika katika mikoa ya Mwanza na Mtwara, awamu ya pili inahusisha  mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mashariki na Magharibi katika mikoa ya Mbeya, Morogoro na Kigoma.

  [caption id="attachment_8578" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki washiriki wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) mara baada ya kufungua semina hiyo leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inahusisha watumishi wa umma kutoka kada za Maafisa Mipango,Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu kutoka Halmashauri na Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe. (Picha zote na: Idara ya Habari – MAELEZO, Mbeya)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi