Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hakuna Mfanyabiashara Atapewa Kibali Kuagiza Sukari Kama Sio Mzalishaji - Waziri Mkenda
Aug 17, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Serikali itasimamia sheria na taratibu iliyojiwekea kwenye usimamizi wa mazao mbalimbali ikiwemo miwa, hivyo haitatoa kibali kwa wafanyabiashara wa sukari badala yake kibali kitatolewa kwa wazalishaji wa ndani kama kutakuwa na uhitaji.


Imebainisha kuwa kwa sasa nchini kuna ziada ya tani zaidi ya 70,000 za sukari hivyo Serikali haiwezi kutoa kibali chochote cha uagizaji wa sukari nje ya nchi wakati uzalishaji unaendelea nchini.


Waziri wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo ya serikali leo tarehe 16 Agosti 2021 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kazi na wazalishaji wakubwa wa sukari hapa nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma.


Amesema kuwa serikali kuendelea kutoa kibali kuagiza sukari nje ya nchi sio sahihi kwani inahatarisha uzalishaji wa sukari nchini jambo linalowakosesha ajira watanzania wengi huku likiwakosesha soko la miwa kwa wakulima ambao miwa yao huchomwa kutokana na uwezo mdogo wa viwanda vya ndani.


“Ninawaomba sana wafanyabiashara wote nchini watambue kuwa serikali inapenda sana wapate faida kwenye biashara zao lakini hii ya sukari waache tupambane ili tuweze kuzalisha ndani ya nchi” Amekaririwa Waziri Mkenda.


Kauli hiyo ya Waziri wa Kilimo inajili wakati ambapo imebainika kuwa kumekuwa na barua nyingi zinazowasilishwa Bodi ya Sukari kwa ajili ya maombi ya kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.


“Mimi ndio msimamizi wa sheria kwahiyo msimuhangaishe sana Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania kwamba yeye anakataa kuwapa ruhusa ya kuingiza sukari, sheria haimruhusu na wala hainiruhusu mimi kutoa kibali hicho”, alisema Mhe Mkenda.


Sheria hiyo imeilekeza Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa sukari iingizwe kwa utaratibu ili kuwekeza Zaidi nchini, hivyo sheria hiyo haitabadilishwa kama watu wanavyofikiri.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Ndg Seif Ally Seif amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia uimarishaji wa viwanda nchini.


Amesema kuwa Uwekezaji wa sukari ni wa muda mrefu hivyo serikali imeendelea kutoa hamasa kwa wawekezaji wa ndani na wa nje katika uwekezaji wa viwanda mbalimbali ikiwemo vya sukari

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi