Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hakuna Aliyeshinikizwa Kujiandikisha Kuhama Ngorongoro
Jun 22, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu – NGORONGORO

Diwani wa Kata ya Eyas iliyopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro amekanusha uzushi unaoenezwa mitandaoni unaodai kuwa jamii za wachungaji zinazoishi kwenye hifadhi hiyo zinashinikizwa kujiandikisha kwenye orodha ya wanaohama kwa hiari kuelekea Kijiji cha Msomera, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Mhe. Augustino Rumay ameyasema hayo leo akizungumza wanahabari katika Kijiji cha Olpiro kilichopo kwenye Kata ya Eyas, Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. 

“Kwa taarifa kabisa nikanushe kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyelazimishwa, nakumbuka kuna watu waliokwenda kwa Mtendaji wa Kata ya Eyas, walipoenda pale na kuitwa wataalamu wa kuja kufanya hili zoezi wakakuta mama na mme wake ndio wanatofautiana lakini hakuna aliyelazimishwa.

“Na hata siku moja mtendaji hajawahi kwenda nyumba ya mtu kumlazimisha mtu kwenda kujiandikisha, mtu mwenyewe kama mimi leo ndio nimemuomba mtendaji wa kata kwamba timu ifike nyumbani kwangu ili nijiandikishe kwa hiari.

“Nimefanya uamuzi huo baada ya kuongea na familia yangu na kuridhia kupokea ombi la serikali, hakuna ulazima wa aina yoyote,” ameeleza Mhe. Rumay. 

Zaidi ya watu 100 wameshahama kutoka kwenye hifadhi hiyo na kuelekea Msomera ambapo wameanza maisha mapya.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi