Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Fuatilieni Wauzaji wa Pembejeo Feki - BRIG. JEN. (MST) Mwangela
Mar 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41296" align="aligncenter" width="720"] Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akizungumza na wadau wa Kahawa kanda ya Mbeya ambayo inajumuisha mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa na Mbeya mapema leo katika Ukumbi wa Khal Hall Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.[/caption]

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Songwe kufanya ufuatiliaji wa wafanyabiashara wanaouza pembejeo feki za kilimo kwa wakulima.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela ametoa agizo hilo mapema leo katika kikao cha wadau wa Kahawa kanda ya Mbeya ambayo inajumuisha Mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa na Mbeya.

[caption id="attachment_41297" align="aligncenter" width="720"] Wadau wa Kahawa kanda ya Mbeya ambayo inajumuisha mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa na Mbeya mapema leo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Khal Hall Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.[/caption]

Amesema kitendo cha mkulima kununua pembejeo feki ni kumsababishia umasikini mkulima huyo jambo ambalo halikubaliki katika Mkoa wa Songwe.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha maafisa ugani wanakwenda kufanya kazi shambani kwa wakulima na sio ofisini, kwani kazi yao kubwa ni shambani.

"Kitendo cha mkulima wa Kahawa kupata robo kilo kwenye mche wa kahawa ni matokeo ya wataalamu wa Kilimo kutowatembelea wakulima mashambani, kwani wenzetu Kenya kwa mche moja wa Kahawa wanapata kilo sita ili swala haliwezekani, kwani sisi tuna ardhi nzuri yenye rutuba na watalamu wapo, hivyo nasisitiza tena watalamu wa kilimo kwenda shambani kwa wakulima", amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela.

Brig. Jen. (Mst) Mwangela amezielekeza Halmashauri zote kuhakikisha zinapanda miche laki mbili ya kahawa ili kuendeleza zao la Kahawa, kwani Kahawa ndio chanzo cha uhakika cha mapato kwa Halmashauri kwa sasa.

Kikao cha wadau wa Kahawa kwa Kanda ya Mbeya kina lengo la kuendeleza zao la Kahawa pamoja na kubadilishana uelewa juu ya mnada wa kahawa ambao utaanza kufanyika kikanda mwaka huu katika Mkoa wa Songwe kwenye Halmashauri ya Mbozi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi