[caption id="attachment_451" align="aligncenter" width="630"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala (kulia) mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisya.[/caption] [caption id="attachment_454" align="aligncenter" width="460"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) leo Jijini Dar es Salaam. Waziri Ummy alimwakilisha Makamu wa Rais katika ufunguzi wa Kongamano hilo.[/caption] [caption id="attachment_457" align="aligncenter" width="630"] Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_460" align="aligncenter" width="578"] Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_463" align="aligncenter" width="508"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_465" align="aligncenter" width="630"] Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(hayupo pichani) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu leo Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_468" align="aligncenter" width="630"] Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala akiteta jambo na Profesa Penina Mrama walipokutana katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.[/caption] [caption id="attachment_469" align="aligncenter" width="630"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawasilisha mada katika Kongamano la Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).[/caption] [caption id="attachment_472" align="alignnone" width="618"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawasilisha mada katika Kongamano la Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia pamoja na baadhi ya waandaji wa kongamano hilo mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
Picha zote na: Frank Shija
Habari na: Anthony Ishengoma - Wizara ya Afya
Uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari umewanufaisha wanafunzi wa kike ambao walikuwa wanakosa fursa hiyo kwasababu baadhi ya wazazi walikuwa wanatoa kipaumbele kwa watoto wa kiume.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akifungua Kongomano la kwanza la Kimataifa la Kijinsia la Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jijini Dar es Saalam.
Waziri Ummy amewataka baadhi ya wananchi kutobeza uamuzi huo kwani unatoa fursa zaidi kwa mtoto wa kike kunufaika na elimu tofauti na awali ambapo baadhi ya familia kwasababu ya umasikini zilitoa kipaumbele kwa mtoto wa kiume.
Aliongeza kuwa kuna madai yakuongezeka kwa idadi ya wanafunzi akisema ongezeko hilo limetokana na kuwepo kwa fursa ya elimu bure ambayo imewezesha watoto walikuwa wanabaki nyum bani kutokana na umasikini kufaidika na uamzi wa serikali ya wamu ya tano kutoa elimu bure.
Amekitaka Chuo Kikuu kishiriki DUCE kufanya utafiti ili kujua watoto hawa waliosababisha ongezeko hilo wanatoka familia za aina gani ili kuiwezesha serikali kuweka mipango endelevu ya utoaji elimu hususani kwa watoto wanaotoka kaya masikini.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuna baadhi ya watu bado wanadhani wazo la kuwarejesha watoto wakike shuleni baada ya kujifungua ni kuhamasisha uhuni akisema lengo la serikali ni kumsomesha mtoto wa kike bila kujali mazingira yanayomzunguka kwasababu watoto wakike kutoka familia tajiri wanapopata ujauzito uhamishiwa na shule binafsi na kuendelea na masomo tofauti na mwanafunzi wakike kutoka kaya masikini.
Katika hatua nyingine amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kudahili wanafunzi wakike kwa asilimia 38 akiwataka kufikia 50 kwa 50 ifikapo 2025 na kuhimiza watoto wakike kushiriki katika masomo ya sayansi kwani takwimu zinaonesha udahili katika masomo ya sayansi katika elimu ya juu bado yako chini ukilinganisha na wanaume.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Pofesa Rwekaza Mukandala wakati akitoa hotuba yake kwa mgeni rasmi amesema kuwa tatizo la unyanyasaji na ukosefu wa fursa sawa kijinsia ni tatizo la kihistoria duniani kote na kusema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitaendelea kufanya tafiti na kutoa elimu ya masuala ya kijinsia ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda mrefu.
Naye Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Profesa William Anangisye amesema tangu kuanzishwa kwa DUCE zimekuwepo juhudi mbalimbali za kuwatafuta wanazuoni kutoka nchi mbalimbali kufika chuoni hapo ili waweze kufundisha na kuzungumzia masuala mbalimbali ya elimu ya kijinsia na usawa katika elimu ya juu.
Amewaambia washiriki kongomano hilo lasiku mbili kuwa kuna washiriki kutoka zaidi ya nchi ishirini na tano na linalenga kutoa matokeo ya tafiti mbalimbali za elimu ya kijinsia kwa jamii na kutoa fursa muhimu miongoni mwa wanazuoni kujadili matokeo ya tafiti hizo.