Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DOMINGOS:Tutaendelea Kuboresha, Kuimarisha na Kuhamasisha Biashara za Mazao ya Kilimo SADC
Aug 11, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46019" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO upande wa Usajili, Bi.Zamaradi Kawawa akiteta jambo na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa SADC, Bi.Barbara Lopi katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Mkurugenzi wa Chakula, Kilimo na Maliasili kutoka Sekritarieti ya SADC, Damingos Dove ulifanyika katika Kituo cha Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46020" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Chakula, Kilimo na Maliasili kutoka Sekritarieti ya SADC, Damingos Dove akifafanua Jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) Kuhusu malengo ya Sekritarieti hiyo katika mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.[/caption]

NA.Mwandishi Wetu-MAELEZO

11-08-2019.

SEKRITARIETI ya Chakula, Kilimo na Malisili kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) imesema kuwa itaendelea kufanya kazi karibu na wananchi walioko kwenye ukanda wa Jumuiya hiyo ili kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya 2015-2020 SADC hasa kwenye Sekta ya Biashara kwa mazo mbalimbali ya Kilimo na Mifugo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Chakula, Kilimo na Maliasili, Domingos Dove alisema kuwa ni vyema kuhusisha vyombo vya habari kwenye sekta hiyo ili kutoa habari zilizohakikiwa, kuona changamoto wanazokumbana nazo, mafanikio ili kili mmoja ajue sekritarieti inakoenda katika kuimarisha biashara na soko la SADC kwenye mazao ya Kilimo na Mifugo.

Alisema kuwa Sekritarieti ina dhamira kubwa ya kutoa wataalamu kwenye kutekeleza sera za Maendeleo za ukanda huo wa Afrika, ili kuhakikisha kunakuwepo na Maendeleo endeelevu kwa nchi wananchama wa Jumuiya hiyo.

[caption id="attachment_46021" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Chakula, Kilimo na Maliasili kutoka Sekritarieti ya SADC, Damingos Dove akifafanua Jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) Kuhusu malengo ya Sekritarieti hiyo katika mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.[/caption]

“Kama Sekritarieti ya SADC tunafanya kazi kubwa kimkakati kwenye nchi wanachama na tunamatarajio makubwa ya kuona na kugusa sehemu zote kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya kanda na kazi hii inahakikisha kwamba sera zote kwenye nchi 16 za Jumuiya hii zinaunganishwa kisera ili kuwezesha kufanya kazi pamoja, hii ndiyo kazi yetu”, Domingos Gove, SADC.

Domingos alisema kuwa malengo ya Sekritarieti hiyo kwa nchi wanachama ni kutangaza, kuunganisha na kuwezesha uunganishwaji wa Sera na miradi mbalimbali ya Maendeleo miongozi mwa nchi 16 wanachama wa SADC.

Domingos alitolea mfano kuwa kama Tanzania itakuwa na program ya Maendeleo kwenye sera ya kilimo, Sekritarieti itafanya kazi ya pamoja na Serikali ya Tanzania ili kuweza kuunganisha sera hiyo kwa nchi zingine 16 za ukanda huo wa afrika.

Alisema kuwa katika kutekeleza sera ya Maendeleo SADC, Sekritarieti hiyo inafanya kazi kwenye maeneo mengi yakiwemo, kuimarisha kilimo na uzalishaji wa mazo ya chakula, kuimarisha eneo la kutangaza biashara na kuwaunganisha wananchi kwenye nchi 16 za SADC ili kuweza kupata soko la watu zaidi ya milioni 300.

“Tunatakiwa kuwa na uwezo wa kutangaza na kuwahamasisha wananchi katika nchi wanachama wa SADC kuzalisha na kuchangamkia soko la zaidi ya watu 300 na hii ndiyo kazi yetu kama Sekritarieti na tutazidi kutangaza, kuboresha na kuhamasisha biashara miongoni mwa nchi wanachama kwenye mazo ya kilimo na Mifugo, kwa hiyo wananchi wanatakiwa kuzalisha kulingana na soko la SADC litakavyokuwa”, Domingos Gove, SADC.

Domingos aliongeza kuwa Sekritarieti hiyo inashughulikia pia masuala ya usalama wa chakula pamoja na lishe bora kwa wananchi kutoka SADC, ili kuwezesha kuwepo na uchumi endelevu katika nchi 16 za Jumuiya hiyo, lengo kuu likiwa ni kuunganisha baadhi ya Sera za Utekelezaji miongoni mwa nchi wanachama.

Aidha, Domingos alisema kuwa Sekritarieti hiyo ina jukumu kubwa la kulinda maliasili zilizoko ukanda huo wa afrika na alitolea mfano kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ulinzi wa maliasili ikiwemo wanyama pori.

“tunajivunia kuwa Serengeti na Kilimanjaro zipo kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika SADC na zinawavutia watu wengi kutoka nchi mbalimbali duniani, tunafurahi kuona Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye ulinzi wa Maliasili ikiwemo mbuga za wanyama Serengeti na Ruaha”, Alisema Domingos Gove, SADC.

Aidha, Sekretarieti hiyo inajukumu la kutekezaji katika kuangalia mabadiliko ya nachi katika ukanda huo wa Afrika kwani hiyo imekuwa ni changamoto kubwa miongoni mwa nchi wanachama wa SADC.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi