Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt.Tulia Kupamba Usiku wa Taarabu
Jun 29, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki - WUSM, Dar Es Salaam

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Akson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Usiku wa Taarabu Julai 03, 2022 utakaofanyika katika Fukwe za Coco (CoCo Beach) Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 29, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla amesema usiku huo utahusisha muziki wa taarabu asilia na taarabu ya kisasa kutoka ndani na nje ya nchi.

“Usiku huu utapambwa na Wasanii wa Taarabu mbalimbali akiwemo Mzee Yusuph, Hadija Kopa, Patricia Hillary, Isha Mashauzi, Sabaha Mchacho, Abdul Misambano na wengine wengi" alisema Mhe. Makalla.

Ameongeza kuwa, vikundi mbalimbali ikiwemo First Class , Wana Nakshi Nakshi, Rahat Zaman, Nadi Ikhwan Safaa, Chama Cha Wasanii wa Muziki Zanzibar pamoja na Vikundi vya taarabu  kutoka nchini  Burundi, Kenya, na. Visiwa vya Comoro vitashiriki

Usiku huo wa taarabu ni muendelezo wa Tamasha la Utamaduni la Kwanza Kitaifa ambalo litafanyika katika Uwanja wa Uhuru Julai 01 hadi 03, 2022 ikiwa ni kuelekea kilelele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi