Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Tax Akutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Comoro
Aug 21, 2023
Dkt. Tax Akutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Comoro
Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed katika ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

 

Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta za kipaumbele hususan biashara na uwekezaji, afya, uchukuzi, elimu, utamaduni, uchumi wa buluu na maeneo mengine.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Comoro. 

“Tanzania itaendelea kushirikiana Comoro ili kuendeleza ushirikiano uliodumu kwa kipindi kirefu kwa maslahi ya pande zote mbili hususan katika sekta za biashara na uwekezaji,” amesema Dkt. Tax

 

Kwa upande wake Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed amesema kwamba Comoro inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania ambapo uhusiano huo umekuwa imara na umedumu kwa muda mrefu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi