Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Mwakyembe Kufungua Mashindano ya Michezo na Sanaa Katika Vyuo Vya Ualimu (UMISAVUTA)
Oct 22, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_48250" align="aligncenter" width="615"] Dkt. Leonard Akwilapo, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia[/caption]

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu kuanza kwa mashindano ya kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara (UMISAVUTA).

Mashindano haya yatafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 31 Oktoba, 2019 Mkoani Mtwara na yatashirikisha washiriki zaidi ya 5,600 kutoka katika vyuo vya ualimu vyote 35 vya serikali.  Ufunguzi wa mashindano hayo unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2019 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) ambaye atakuwa anamwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Michezo itakayoshindaniwa ni pamoja na Mpira wa Pete, Mpira wa Miguu, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Riadha. Pia, kutakuwa na mashindano ya uchoraji, sanaa za maonesho na ngoma pamoja na kwaya na mashindano ya kutengeneza zana za kufundishia.

Baada ya ufunguzi huo michezo hiyo itaendelea katika viwanja vya michezo vya Chuo cha Ufundi Mtwara na Chuo cha Ualimu Mtwara na yanategemewa kufungwa Oktoba 31, 2019 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Lazaro Ndalichako.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi