Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Mwakyembe: BMT Waiteni TASWA Kujadili Katiba Kabla ya Uchaguzi Mkuu
Oct 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36292" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari za michezo kilichofanyika jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo.[/caption]

Na: Lorietha Laurence –WHUSM,Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuitisha kikao na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA)  pamoja na baadhi ya waandishi wa habari hizo kujadili na kupitia katiba ya chama hicho.

Dkt. Mwakyembe ametoa rai hiyo jana Jijini Dar es Salaam alipokutana na baadhi ya Waandishi wa Habari za michezo , alichokiitisha baada ya kupokea barua ya malalamiko  zinazoelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili waandishi hao wa michezo.

[caption id="attachment_36293" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wasanii wa Nafasi Arts Space alipowatembelea jana ofisini kwao Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_36294" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya Waandishi wa Habari za michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika picha) katika kikao kilichofanyika jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.[/caption]

“ Watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa  waiteni viongozi wa TASWA wakiwemo na wawakilishi ambao ni waandishi wa habari za michezo  ili kupitia katiba inayokiongoza chama hicho kabla ya uchaguzi Mkuu” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aliongeza kwa kueleza kuwa waandishi wa habari za michezo wana uhuru wa kuunda chama kipya endapo hawaridhishwi na utendaji wa TASWA ingawa kabla ya kufanya maamuzi yoyote, kikao kifanyike kwanza ili kufikia muafaka.

Alizidi kufafanua kuwa  waandishi wa habari za michezo ni muhimili muhimu katika sekta ya habari na maendeleao ya michezo  ndani na nje ya nchi, kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha jamii  kuhusiana na masuala ya michezo.

[caption id="attachment_36295" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akipata maelekezo kutoka kwa Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Bw. Ramadhani Mabera (kushoto) na kulia ni Mwalimu wa Sanaa za Uchoraji kutoka Zanzibar Bw. Abdulla Omar maarufu kama Dulla Wise.[/caption] [caption id="attachment_36296" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akipokea zawadi ya picha ya kuchora kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Nafasi Arts Space Bibi. Sauda Simba baaada ya kuzungumza na wasanii hao jana Jijini Dar es Salaam[/caption] [caption id="attachment_36297" align="aligncenter" width="800"] Mjumbe wa Bodi ya Nafasi Arts Space Bibi. Sauda Simba (Kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea kikundi hicho cha sanaa za ufundi na maonyesho kilichopo Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_36298" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Wasanii wa Nafasi Arts Space baada ya kufanya ziara na kuzungumza nao jana katika ofisi zao zilizopo Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Dar es Salaam).[/caption]

Wakati huo huo, Dkt. Mwakyembe alipata nafasi ya kutembelea wasanii wa kikundi cha Nafasi Arts Space kilichopo Mikocheni B Jijini Dar es Salaam, ambapo alifurahishwa na kazi mbalimbali za sanaa zinazofanywa na kikundi hicho.

“Nimefurahishwa na ubunifu unaofanywa mahali hapa kwa hakika nafasi arts space ni jukwaa muhimu  la  sanaa ambalo linatoa fursa ya ajira kwa vijana ”alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha aliwataka wasanii hao kukutana kwa pamoja na kupitia Katiba inayoongoza kikundi hicho kwa ajili ya kutoa maoni mbalimbali yatakayosaidia kuboresha katiba hiyo kwa utendaji mzuri zaidi.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Nafasi Arts Space Bibi. Sauda Simba aliahidi kufanyia kazi maagizo hayo kwa hakikisha wasanii wanapitia katiba hiyo na kutolea maoni na kutoa mrejesho kwa kile walichokubaliana.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi