Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa salaamu za pole za Serikali na Wizara yake leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari, marehemu Muhingo Rweyemamu aliyefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Akitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali na Wizara yake leo Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mwakyembe amemuelezea marehemu Rweyemamu kuwa alikua mtumishi mzuri katika Serikali hasa katika wadhifa wake wa Ukuu wa Wilaya na mara zote alihakikisha Wananchi anaowaongoza wanakuwa wachapakazi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
“Serikali inatoa pole sana kwa familia na wanatasnia ya habari kwani marehemu Rweyemamu ameacha pengo kubwa kwa familia yake na wanahabari kutokana na uhodari wake katika uandishi lakini pia Serikali inakumbuka uchapakazi wake alipokua Serikalini. Tunaomba Mungu awape faraja na uvumilivu wafiwa wote”. Alisema Mhe. Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe amemuelezea marehemu kuwa alikuwa mchapakazi hodari wakati alipokuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na Wananchi wa Handeni watamkumbuka katika jitihada zake za kuhimiza watoto wa kike kupenda shule ambapo alianzisha kampeni iliyoitwa “niache nisome” lengo likiwa ni kuelimisha umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.
“Wananchi wa handeni wamesikitishwa sana na kifo hiki kwani wanakumbuka uhodari wake katika kuwatumikia alipokuwa mkuu wa Wilaya yao hasa juhudi zake za kuhimiza jamii kupeleka watoto shule kwa manufaa yao ya baadae”. Alisema Mhe. Gondwe”.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Naye mwakilishi kutoka vyombo vya habari Bw. Absolum Kibanda amesema kuwa marehemu alikuwa mwalimu na mshauri mzuri katika tasnia ya habari na alikuwa anaipenda kazi yake na kufanya waandishi wengi kuiga na kujifunza kutoka kwake uandishi wa habari za uchunguzi na makala.
Marehemu Muhigo Ryeyemamu amewahi kufanya kazi katika magazeti ya mbalimbali hapa nchini ikiwemo Mtanzania, Mwananchi, Rai, The Citizen akitumikia nyadhifa mbalimbali kama mhariri na mwandishi. Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na ameacha mke,watoto wanne na mjukuu mmoja.
Baadhi ya waombolezaji wakifuatilia tukio la kuaga mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bibi Sophia Mjema akitoa heshima za mwisho leo Jijini Dar es Salaam kwa mwili wa Mkuu wa Wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.
Mtoto wa marehemu Muhingo Rweyemamu Bw. Emmanuel Muhingo akisoma wasifu wa baba yake aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan wakati wa kuagwa leo Jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw.Godwin Gondwe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa mkuu wa wilaya mstaafu na Mwanahabari Marehemu Muhingo Rweyemamu aliefariki Septemba 2 mwaka huu katika hospitali ya Agha Khan.