Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Magufuli: Sekta ya Sanaa na Michezo kuongezewa Nguvu Zaidi Miaka Mitano Ijayo.
Jun 16, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53233" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza  leo Jijini Dodoma, wakati wa shughuli za kuvunja Bunge la kumi na moja.[/caption]

Na. Shamimu Nyaki - WHUSM

Serikali imeahidi kuweka mkazo na kuongezea nguvu zaidi  sekta  za Sanaa na Michezo nchini kwa  kipindi  cha miaka mitano ijayo, hiyo inatokana na mchango mkubwa unaofanywa na wasanii na wanamichezo ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza  leo Jijini Dodoma, wakati wa shughuli za kuvunja Bunge la kumi na moja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   ameeleza kuwa shughuli za sanaa na michezo zimekua mstari wa mbele  katika kuburudisha,kukuza uchumi na kutangaza nchi kimataifa.

“Kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na wasanii na wanamichezo,Serikali imejipanga katika miaka mitano ijayo kuweka mkazo wa nguvu kwenye sekta hizi  ambazo zimeajiri vijana wengi”alisema Dkt.Magufuli.

Dkt.Magufuli ameongeza kuwa sekta ya Sanaa na burudani ziliongoza kwa ukuaji katika mwaka 2018 ambapo sekta hii ilikua kwa asilimia 13.7 na mwaka 2019 ilishika nafasi ya tatu kwa ukuaji wa asilimia 11.21 huku akiwapongeza wasanii hususani  wa muziki wa kizazi kipya,filamu na wachezaji wa soka kwa kuchangia uchumi wa nchi.

Aidha Dkt.Magufuli ameipongeza timu ya Taifa ya mpira wa miguu ambayo kwa mwaka 2019, ilifanikiwa kufuzu kushiriki mashindano ya fainali za Kombe la Afrika ikiwa ni historia baada ya kushindwa kufika huko kwa takribani miaka 39 huku akieleza kuwa mchezo wa ndondi na riadha umeipeperusha vizuri bendera ya nchi yetu.

Vilevile Mhe.Rais Magufuli  ameeleza kuwa nchi yetu imeaminiwa katika kuongoza Kanda mbili ikiwemo Jumuiya ya Nchi za  Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo pamoja na mafanikio iliyoyapata katika uongozi huo ni kuweza kuzishawishi nchi wanachama kuridhia lugha ya Kiswahili kutumika kwenye taasisi hizo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi