Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt.Jafo: Tanzania Kinara Usimamizi wa Biashara ya Hewa Ukaa
Nov 12, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema katika Mkutano 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27), Tanzania imekuwa ni nchi kinara katika uandaaji wa Mwongozo wa Biashara ya Hewa ya Ukaa.

Amesema hayo leo Novemba 12, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi. Zuhura Yunus na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini China na Misri hivi karibuni.

Dkt. Jafo alisema hapo mwanzo hatukuwa na Kanuni wala Mwongozo wa biashara hii na hivi sasa kukamilika kwake kutasaidia Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari alisema anamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyeungana na wakuu wengine wa nchi zinazoendelea kupaza sauti kuzitaka nchi zinazoendelea kutimiza wajibu wao.

“Ni kweli changamoto ya uzalishaji wa hewa ukaa ni kubwa na nchi yoyote duniani inapofanya uchafuzi huo wa hewa zinaathrika nchi zote duniani na ndio maana wataalamu wanatuambia ifikapo mwaka 2050 kuna uwezekano barafu katika Mabara mbalimbali katika milima ukiwemo Kilimanjaro zitayeyuka kutokana na ongezeko la joto,” alisema.

Waziri Jafo alisema kutokana na hali hiyo, Mkutano wa Paris wa mwaka 1992 uliazimia nchi zinazoendelea ambao ndio wazalishaji wakubwa wa hewa ukaa wanapaswa kuchangia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 100 kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Kutokana na msukumo mkubwa kwa nchi zinazoendelea kutakiwa kutoa fedha, tayari katika awamu iliyopita Tanzania ilipokea Dola za Marekani milioni 23.6 na kwa mgao unaotarajiwa kutolewa tutapata Dola za Marekani milioni 52.8 na hii ni kutokana na jitihada zilizofanyika katika Mkutano uliopita wa COP26,” alisema. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi