Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Abbasi Akutana na Kufanya Mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO
Feb 21, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28904" align="aligncenter" width="640"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa akipata maelezo ofisini kwake jijini Dar es Salaam; kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dakta Hassan Abbasi, kuhusu majukumu ya Idara ya Habari Maelezo na Mfumo wa Upashanaji Habari na Mawasiliano Serikalini (Picha kwa hisani ya STAMICO).

[/caption] [caption id="attachment_28902" align="aligncenter" width="640"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dakta Hassan Abbasi (kushoto) akikabidhi Jarida la NchiYetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Jarida hilo linaratibiwa na Idaraya Habari Maelezo.[/caption]

Na Koleta Njelekela, STAMICO

Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Mhandisi John Nayopa amekutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dakta Hassan Abbasi, ambaye alifika katika Ofisi za Makao Makuu ya STAMICO jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamia na naye nakuzungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano katika upashanaji habari za STAMICO kwa Watanzania.

Viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika sualazima la kuelimisha Watanzania kuhusu shughuli za STAMICO kwa kutumia mitandao ya kijaamii (Social Media) ya Idara ya Habari Maelezo, Jarida la Nchi yetu linaloratibiwa na  Idara hiyo na Vyombo vya Habari kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dakta Abbasi amesema Idara yake iko tayari kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa STAMICO katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji yao, ilikuwajengea uwezo zaidi katika taaluma zao.

[caption id="attachment_28903" align="aligncenter" width="561"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali,Dakta Hassan Abbasi (kushoto) akitoa maelezo kwa ufupi kuhusu Jarida la NchiYetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.[/caption]

“ Kulingana na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Idara yangu inaweza kutoa mafunzo ya kuanzia kwa wataalamu wako kuhusu Sayansi ya Mitandao ya Kijamii na uendeshaji wake; Mawasiliano kwa Umma wakati wa Majanga (Crisis Communication);pamoja na Sera na Miongozo ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii” Alifafanua Dakta Abbasi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Nayopa amemshukuru Dakta. Abbasi kwa kumtembelea ofisini kwake na ameahidi kuimarisha ushirikiano na Idara ya Habari Maelezo katika kuelimisha Watanzania kuhusu mchango wa STAMICO katika kuleta matokeo chanya kwenye Serikali ya awamu ya tano.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi