Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DC Gairo Asimamisha Uchimbaji Madini bila Leseni
May 14, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kutembelea sehemu ya migodi inayochimbwa kinyemela na wachimbaji wasiokuwa na leseni.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe amesikitishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya viwandani wanaochimba madini mbalimbali Wilayani hapo hasa aina ya Felispar bila leseni.
Mhe. Mchembe aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kata ya Rubeho ambapo wachimbaji wameweka mashine nzito na wanafanya kazi wakati hawana leseni.
Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kifungu cha 18 kimeweka bayana adhabu kwa mchimbaji haramu. ikiwa ni mtu binafsi faini isiyozidi milioni 5 au kifungo miaka mitatu au vyote pamoja na kama ni kampuni basi ni faini isiyozidi shilingi milioni 50.
Mheshimiwa Mchembe aliendelea mbali na kuelezea kifungu cha 6 (4) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji namba 29 ambapo madini yaliyopatikana kupitia uchimbaji haramu yatataifishwa na Serikali chini ya Kamishna wa madini na kuuzwa kwa mnada. Mitambo yote pia inapaswa kutaifishwa.
Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Mchembe ametoa maagizo hayo na kumtaka Afisa Madini Mkoa na Kanda kufatilia jambo hilo kwa karibu.
Pia amepiga marufuku raia wa kigeni kutembelea maeneo ya machimbo bila kibali. Aidha uzingatiwaji wa kanuni 3 (1) (2) ambapo mchimbaji anatakiwa kuwasilisha kwa Afisa Madini mkazi kanda taarifa ya tathmini na mpango wake wa utunzaji wa mazingira kabla ya kuanza kuchimba madini.
Wilaya ya Gairo ina madini aina mbalimbali na maeneo ya milimani yameachwa na mashimo makubwa.

Moja ya mashine zilizokutwa eneo la mgodi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi