Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DC Chemba: Taarifa Mnazokusanya Zitaisadia Wilaya yetu Kujipanga Vyema
May 26, 2020
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_52759" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza na ujumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliyoongozwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa wakati ulipokuwa wilayani humo kukagua maandalizi ya Sensa ya Watu na Mkazi ya Mwaka 2022.[/caption]

Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Simon Odunga amepongeza kazi nzuri ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu inayofanywa na wataalamu wa Mifumo ya Taarifa ya Kijiografia (GIS) kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS).

Mkuu wa Wilaya huyo alitoa pongezi hizo ofisini kwake hivi karibuni wakati alipokuwa akizungumza na wataalamu hao wakiongozwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa ambao walimtembelea.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Chemba kukagua ubora wa kazi ya utengaji maeneo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanya mwaka 2022.

[caption id="attachment_52757" align="aligncenter" width="750"] Mrasimu Ramani Martha Macha akimuonesha kitu Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa wakati wa kuhakiki kazi ya utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu ikiwa ni maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 huko wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.[/caption]

Bwana Odunga amesema kwa kuwa tekinolojia inayotumiwa sasa katika kutenga maeneo inawezesha kuchukua taarifa nyingi ikiwemo miundombinu ya barabara, huduma za afya, maji, elimu na ofisi mbali mbali za serikali tangu ngazi ya kijiji hadi wilaya, taarifa hizo zitaisaidia sana wilaya katika kupanga mipango ya maendeleo katika ngazi mbalimbali.

“Nimefurahishwa na kazi yenu ambayo mbali ya kutenga maeneo lakini taarifa mnazokusanya zitausaidia uongozi wa wilaya yetu kuielewa vyema wilaya hivyo zitatusaidia kujipanga vyema na kwa weledi katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na masuala mengine ya kimaendeleo” alisema Bwana Odunga.

Alisifu utendaji bora wa timu hiyo na namna ilivyoweza kuyafikia hadi sasa maeneo mengi katika wilaya hiyo pamoja na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo wilayani humo huku nchi ikiwa katika kipindi cha mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi hatari vya Corona.

Mkuu wa Kitengo cha Mfumo wa Taarifa za Kijiografia wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Benedict Mugambi akimueleza Mtakwimu Mkuu wa Serikali namna kazi ya utengaji maeneo kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi inavyoendelea wilayani Chemba. Kulia ni Mrasimu Ramani Martha Macha na Mtakwimu Mkuu Seif Kuchengo.

“Wilaya yetu bado ni mpya; tuna changamoto nyingi hasa upande wa miundombinu ya barabara lakini mnafanya kazi kwa umahiri mkubwa na kuweza kufika kila kitongoji, kijiji, kata na tarafa” alibainisha na kuongeza kuwa wilaya hiyo ina vijiji 114, kata 26, tarafa 4 na vitongoji 498.

Bwana Odunga alisisitiza umuhimu wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa kubainisha kuwa takwimu zitakazokusanywa katika Sensa hiyo zitaiwezesha Serikali kufanya mapitio ya Dira ya Maenddeleo 2025 ambapo lengo lake ni kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kipato cha na pia msisitizo wa utekelezaji wa mpango wa taifawa kujenga uchumi wa viwanda.

Kwa upande wa wilayani kwake alieleza kuwa wakati wote wanawasisitizia viongozi katika ngazi zote umuhimu wa matumizi ya takwimu katika kufanya maamuzi yanayohusu maendeleao ya wananchi.

“Kiongoni mathalan wa kijiji ambaye haelewi mipaka ya kijiji anachokiongoza kiutawala, haelewi kuna kaya ngapi, hajui idadi ya wanawake na wanaume, hajui idadi ya vijana itakuwa vigumu uongozi wake kutoa matokeo bora” Alisisitiza.

[caption id="attachment_52761" align="aligncenter" width="750"] Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa akizungumza na viongozi wa Kijiji cha Chemba pamoja na timu ya wataalamu wa utengaji maeneo ya kuhesabia watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu baada ya kukagua ubora wa kazi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.[/caption]

Wakati huo huo Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Albina Chuwa alimueleza Mkuu wa Wilaya huyo kuwa ziara yake Wilayani humo ni kukagua ubora wa kazi inayofanyika ya kutenga maeneo madogo madogo ya kuhesabia watu kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.

Alieleza kuwa sehemu kubwa ya kazi hiyo katika wilaya ya Chemba imekamilika isipokuwa sehemu ndogo tu ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

“Leo tutapitia baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa kazi katika kijiji cha Chemba hapa kitongoji cha Shuleni ili kuyahakiki na tutakapokamilisha kazi hivi karibuni tutakukabidhi taarifa ili viongozi wa wilaya nanyi mjiandae tayari kwa Sensa” alieleza.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali alieleza kuwa kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu itafanyika hatua kwa hatua katika wilaya zote 139 na halmashauri zote 185 nchini ili kuhakikisha Sensa inafanyika katika kiwango cha ubora unaokubalika.

Alibainisha kuwa lengo kuu ni kuhakikisha watu wote wanahesabiwa na kunakuwepo na takwimu tangu ngazi ya kaya hadi ngazi za juu ambazo zitasaidia Serikali na wananchi kwa pamoja kupanga mpango ya Maendeleo.

Naye mkuu wa kitengo cha Mfumo wa Taarifa za Kijiografia Benedict Mugambi alieleza kuwa kazi ya kutenga maeneo katika mkoa wa Dodoma imekamilika katika Wilaya za Chamwino, Bahi na Kondoa ambapo watakapokamilisha sehemu ndogo ya kazi iliyobaki wilaya ya Chemba wataalamu hao watakwenda wilaya nyingine zilizobaki mkoani humo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi