Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DAWASA yaendelea kutekeleza Operesheni ya kuzui uvujaji wa maji
Oct 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36381" align="aligncenter" width="576"]  Mafundi wa Mamlaka ya MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na Operesheni ya kuziba mabomba yanayovuja maji katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi. Operesheni ya kuzuia maji kuvuja tayari imefanyika Tegeta na leo inaendelea katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na;  Mwandishi wetu

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imeanzisha Operesheni maalum  ya kupambana na uvujaji wa maji katika Jiji hilo ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha   huduma zake kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo  , Dhamira ya Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa inaondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji kwa kuzuia maji yasivuje kutoka katika mabomba hali itakayoongeza tija katika huduma zinazotolewa kwa wananchi na kuongeza mapato ya Mamlaka hiyo.

"Kazi hii inahusisha mafundi zaidi ya 70 na lengo ni kupunguza tatizo la maji kuvuja kwa asilimia 90 katika maeneo yote DAWASA inayotoa huduma "; Inasisitiza sehemu ya taarifa hiyo

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Kazi hiyo inayosimamiwa na Idara ya Uzalishaji  na Usambazaji Maji itatekelezwa kwa weledi wa hali ya juu ili kufikia lengo la kuzuia upotevu wa maji kutokana na kuvuja.

Katika kuimarisha huduma zake kwa wananchi DAWASA imejidhatiti kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Mamlaka hiyo, yakiendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge.

Aidha, Mamlaka hiyo imekwishaendesha Operesheni ya kudhibiti uvujaji wa maji katika eneo la Tegeta na sasa zoezi hilo linaendelea kuanzia leo Oktoba 6, 2018 katika  eneo la Magomeni na katika maeneo mengine Jijini Dar es Salaam na Pwani.

Mamlaka ya Maji Safi na Maji  Taka Dar es Salaam (DAWASA) imefanikiwa katika kuboresha huduma zake kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa upatikanaji wa maji ni wa uhakika na unaendana na mahitaji ya wananchi na dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi