Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

DARUSO Yampongeza JPM kwa Kulinda Rasilimali za Nchi.
May 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_1967" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam ukilenga kutoa tamko la DARUSO kuhusu kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali hasa matokeo ya Tume ya kuchunguza kiwango cha madini kwenye makontena 277.Kulia ni Waziri wa Ulinzi wa Serikali hiyo Bw. Richard Augustine na kushoto ni Waziri Mkuu wa Serikali hiyo Bw. Sintau Fredrick.[/caption]

Na Frank Mvungi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (DARUSO) kwa kusimamia vyema rasilimali za Taifa ili ziweze kuwanufaisha watanzania wote.

Kauli hiyo  imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na  Rais wa (DARUSO) Bw.John Jilili wakati wa mkutano wao na vyombo vya habari uliolenga kutoa tamko la kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais kwa kuunda Tume iliyochunguza na kutoa matokeo kuhusu mchanga (makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi.

Kuanzia  sasa uchakataji (processing) ufanyike hapa nchini na mikataba yote iwe na kipengele kinachoyalazimisha makampuni yanayopewa leseni ya kuchimba madini kuwa na mitambo ya kuchenjua makinikia ya madini yanayozalishwa na migodi hiyo.” alisema  Jilili

[caption id="attachment_1968" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) akitoa tamko lao mbele ya waandishi wa Habari kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano katika kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika na rasilimali za madini.kushoto ni Waziri Mkuu wa Serikali hiyo Bw. Sintau Fredrick.[/caption]

Akifafanua zaidi Jilili amesema kuwa mikataba yote ya Madini ni vyema ikatazamwa upya na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa na si ya watu wachache, kwani kwa kufanya hivyo kuonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuleta mageuzi katika sekta ya madini nchini.

Katika mapendekezo yao DARUSO imebainisha kuwa Watanzania wangependa kuona Mikataba na Sheria zilizopo zinaruhusu ukaguzi wa mara kwa mara migodini ili Serikali ijiridhishe kuhusu kiwango cha madini kinachozalishwa katika migodi hiyo pamoja na Serikali kuwa na ubia wa asilimia 50 au 49 na wawekezaji katika sekta ya madini.

Aidha Jilili alisema vyema pia kwa vyema kwa Viongozi wote waliopewa dhamana ya kuwaletea wananchi maendeleo wakatekeleza wajibu huo kwa uzalendo na kuepuka kuingia mikataba inayowezesha kuiletea hasara Serikali.

“Tunapenda kuwaomba watanzania wote wasomi na wasio wasomi kumsaidia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufikia lengo lake la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na hayo yanawezekana tu kwa kuweka uzalendo mbele na maslahi ya Taifa kwanza.” Alisisitiza Jilili

Aliongeza kuwa nidhamu na uwajibikaji katika sehemu za kazi ni jambo la muhimu kwa Watendaji waliokabidhiwa majukumu ya kusimamia sekta mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo  kutawezesha kuzaliwa kwa Tanzania mpya chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano.

“DARUSO inamthibitishia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Watanzania wote kuwa iko sambamba nae katika harakati zake za kuikomboa nchi yetu katika Nyanja zote ikemo kiuchumi” Alisisitiza Jilili.

DARUSO haishangai juu ya matokeo ya tume iliyoundwa na Mhe. Rais Magufuli kwani inaamini kuwa kama utafiti haupo basi hakuna haki ya kuongea chochote.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi