Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Daraja la Wami Kukamilika ndani ya Miezi 24
Nov 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

Frank Mvungi

Serikali kutumia  zaidi ya Bilioni 67 katika ujenzi wa Daraja la mto Wami na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 na hivyo kuchochea  ukuaji wa sekta ya uchukuzi hapa nchini.

Akijibu swali la kuhusu ujenzi wa Daraja hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe.  Elias Kuandikwa amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi ambapo baada ya maandalizi hayo kazi ya ujenzi wa daraja utaanza ukigharimiwa na Serikali kwa asilimia 100.

“ Wakati wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi   Power Construction Corporation kutoka China walisaini mkataba wa ujenzi wa daraja hili tarehe 28/05/2018 hivyo tayari kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza wakati wowote”; Alisisitiza Mhe. Kuandikwa

Akifafanua Mhe. Kuandikwa amesema kuwa Daraja jipya la Wami litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litajengwa umbali wa mita 670 pembeni ya daraja la zamani upande wa kulia  ukiwa unaelekea Segerea.

Aliongeza kuwa upana wa daraja hilo umezingatia sehemu ya barabara, waenda kwa miguu pamoja na vizuizi kwa ajili ya usalama.

 Daraja hilo litakuwa kichocheo cha maendeleo katika mikoa ya Kaskazini  kwa kuchochea shughuli za usafirishaji na uchukuzi kwa njia ya barabara.

Daraja la  sasa la mto Wami lenya urefu wa mita 88.75 liko mkoa wa Pwani na lilijengwa mwaka 1959 na ni kiungo muhimu kutoka Chalinze kwenda mikoa ya ukanda wa Kaskazini mwa nchi yetu na nchi za jirani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi