Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Chavita Kutumia Milioni 80 Kuelimisha Umma.
Sep 06, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_12289" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Bi. Nidrosy Mlawa(kulia) akieleza jambo kwa lugha ya alama alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mradi wa uwezeshaji Viziwi kwa mikoa ya Arusha, Mwanza na Morogoro leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na: Paschal Dotto

Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kitatumia zaidi ya shilingi milioni 80, kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhusiana na haki za viziwi na kutoa mafunzo kwa watendaji wa Serikali za Mitaa katika mikoa ya Morogoro Mwanza na Arusha.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na  Mratibu wa Miradi wa Chama hicho Msafiri Mhando  wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu Mradi wa kuelimisha jamii katika masuala ya viziwi kushiriki katika maendeleo na kupata haki za msingi kama raia wengine.

Mhando  amesema kuwa mradi huu umefadhiliwa na asasi ya The Foundation for Civil Society (FCS) na kwa kuanzia unategemea kuwafikia watu 900 wakiwemo viziwi 600 na watendaji 300.

Aidha, Mhando aliongeza kuwa mradi huo utaendelea kuwafikiwa watanzania wengine hususani mkoa wa Singida hasa maeneo ya vijijini ambako ufahamu wa haki za viziwi pamoja na matumizi ya lugha za alama uko chini.

“Kama tunavyo fahamu viziwi wanaishi katika jamii ya watanzania kama ilivyo kwa walemavu wengine, tunachoangalia hapa ni nini kinajitokeza katika maisha ya kila siku ya viziwi hawa na kutoa msaada, chama hiki kinawajibu huo”, alisema Mhando.

Akizungumzia umuhimu wa elimu hiyo Mhando alisema kwamba asilimia 20 ya walemavu wote tanzania ni wenye ulemavu wa kutokusikia hivyo basi kundi hili ni muhimu likapewa kipaumbele katika masuala ya mawasiliano hasa matumizi ya lugha za alama.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho Nidrosy Mlawa amewaasa watanzania wenye tatizo hilo wajitokeze ili kuweza kuwapa taarifa kamili na kujua idadi ya viziwi tanzania.

“watu wengi wenye tatizo hili hasa wanaopatwa na tatizo ukubwani wamekuwa na tabia ya kujificha na kujifanya kama siyo viziwi jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa takwimu kamili ya viziwi Tanzania”. Alisema Nidros

Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1983 na kusajiliwa rasmi 1984 chini ya Sheria ya vyama vya hiyari namba 5 ya mwaka 1954 na kwa sasa inaendelea na jukumu la kusimamia haki za viziwi nchini ikiwa ni pamoja na kupigania usawa na katika jamii ili viziwi waweze kupata maendeleo katika nyanja zote za elimu, uchumi, siasa, ajira na haki ya kupata habari.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi