Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bonanza la Michezo Kufanyika Kila Baada ya Miezi Miwili
Oct 06, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_47770" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi wetu – WHUSM,Dodoma.

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo amesema kuwa Bonanza la Michezo litaendelea kufanyika kila baada ya miezi miwili  na litahusisha michezo mbalimbali.

Bw.Singo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipozungumza wakati akishukuru Watumishi wa Serikali na wananchi wa Jijini la Dodoma waliojitokeza kushiriki Bonanza hilo.

[caption id="attachment_47771" align="aligncenter" width="1000"] Muongozaji wa mazoezi Bw.Simba akiongoza mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47773" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Watumishi wa Serikali na wananchi wa jiji la Dodoma wakifanya mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47774" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Watumishi wa Serikali na wananchi wa jiji la Dodoma wakifanya mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47775" align="aligncenter" width="871"] Timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ikiwa uwanjani ikishindana na timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo timu hiyo iliibuka kidedea katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47776" align="aligncenter" width="977"] Timu za Mpira wa miguu za Serikali na Baobao Queens ya Jijini Dodoma zikichuana vikali katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma ambapo timu ya Serikali ilishinda kwa magoli matatu dhidi ya goli moja.[/caption]

“Bonanza hili litafanyika kila baada ya miezi miwili lengo ikiwa ni kuimarisha afya zetu pamoja na kuimarisha upendo,amani na mshikamano tulionao Tanzania”alisema Bw.Singo.

Aidha Bw.Singo amesema kuwa Bonanza hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo  mbio za taratibu,mazoezi ya viungo, mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na michezo mingine.

Naye Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Daudi Manongi amesema kuwa Bonanza hilo limekuwa na faida nyingi kwani  limewakutunisha Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Jiji la Dodoma katika kuimarisha afya zao na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza kazi zao.

Katika bonanza hilo timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya habari,Elimu na timu ya Joggin kutoka Dodoma ziliibuka washindi ,huku timu ya mpira wa miguu ya Serikali ikiifunga magoli matatu timu ya Boabao Queens ya Jiji la Dodoma iliyoambulia goli moja.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi