Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Balozi Kijazi Aiomba ERB Ikapitie Upya Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2016
Sep 05, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34855" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia), akitoa utambulisho kwa wahandisi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption]

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameitaka Bodi ya Usajili ya Wahandisi nchini (ERB) kuipitia upya Sheria ya manunuzi ya mwaka 2016 ili kuweza kubaini changamoto zilizopo katika sheria hiyo kuhusu fursa  za wakandarasi wazawa kushiriki kikamilifu  katika ujenzi wa miradi mikubwa ya Serikali.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo jijini Da es salaam, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika  ufunguzi wa  Kongamano la Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Wahandisi sambamba na Siku ya Wahandisi nchini linalofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi aliitaka Bodi ya Wahandishi (ERB)  kuhakikisha kwamba   inaisoma upya Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016 ili kubaini changamoto zilizopo badala ya kulalamika kuwa Serikali haiwashirikishi kikamilifu wakandarasi wazawa.

[caption id="attachment_34865" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wahandisi wakimsikiliza Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34864" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wahandisi wakimsikiliza Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption]

“Nawaomba ERB  mkaisome upya Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016, ambayo ilifanyiwa marekebisho  hasa vifungu  vya 55A, 55B, 55C na 55D ili kufahamu kwa kina jinsi sheria hiyo ilivyoainisha utaratibu wa kampuni za ndani katika miradi ya ujenzi, ili kubaini mapungufu yaliyopo na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha zaidi badala ya kulalamika kuwa Serikali haiwashirikishi kikamilifu katika miradi ya mikubwa ya nchi”

Balozi Kijazi, alisisitiza kuwa Serikali iko tayari kupokea mapendekezo hayo na  itarekebisha sheria hiyo kulingana na maoni yatakayotolewa.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika kazi za kihandisi, hasa ukilinganisha kuwa kabla ya Uhuru nchi hii ilikuwa na wahandisi wawili tu, lakini hadi sasa ERB imesajili jumla ya Wahandisi 22,226 kati yao wakiwemo wahandisi wanawake 22,235 sawa na asilimia 10.

[caption id="attachment_34863" align="aligncenter" width="923"] Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia) akimkabidhi tuzo ya heshima moja ya mjumbe wa kwanza wa Bodi ya Usajili Wahandisi, Mhandisi Anase Shayo wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34862" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kushoto) akipokea saa toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Profesa Ninatubu Lema (kulia) kwa niaba ya Rais John Magufuli wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34861" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akimkabidhi tuzo ya heshima Mhandisi Milton Nyerere kwa niaba ya familia ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kutambua mchango Baba wa Taifa katika kuanzishwa kwa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption]

Naye, Rais wa Shirikisho la Wakandarasi Afrika, Julius Riunga alizitaka Serikali za nchi za kiafrika kuwaunga mkono wakandarasi ili waweze kuendeleza ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendelo kwa wananchi. Ambapo pia alisisitiza  kuwa Afrika itajengwa na wandarasi  wa kutoka Afrika.

Aidha, amewataka wakandarasi kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo katika nchi zao, ikiwa ni pamoja na kuliletea maendeleo bara la Afrika kwa ujumla.

Kwa upande wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Trygve Bendiksby alisema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika  miradi mbalimbali ikiwemo  ufadhili wa mafunzo kwa wakandarasi wanawake  463 hadi sasa, kutika wakandarasi 96 waliokuwa mwaka 2010.

[caption id="attachment_34860" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34859" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akimkabidhi tuzo ya heshima Naibu Balozi wa Norway Tanzania Trygve Bendiksby wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34858" align="aligncenter" width="1021"] Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akizungumza na wahandisi na wakandarasi wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34857" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kuzungumza na wahandisi na wakandarasi wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption] [caption id="attachment_34856" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB), Profesa Ninatubu Lema (kulia) akitoa neon la utangulizi kwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kusheherekea miaka 50 ya Bodi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1968.[/caption]

Balozi  Bendiksby, alisisitiza kuwa “Norway ni mshirika mzuri wa maendeleo na tutaendelea kufanya hivyo, tunaona mabadiliko makubwa na watu wanafaidika na juhudi za kupambana na rushwa zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli”

Aidha, katika Maadhimisho hayo ya miaka 50 ya ERB, zimefanyika shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa tuzo kwa kutambua michango ya watu mbalimbali walioshiriki katika shughuli za kihandisi kwa kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo.

Kati ya waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliyetunukiwa tuzo maalumu iliyopokelewa na Milton Nyerere kwa niaba ya familia yake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ambao walitunukiwa tuzo za heshima kwa michango yao ya taaluma katika sekta ya ujenzi nchini.

Kongamano hilo la Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Wahandisi na Siku ya Wahandisi mwaka huu inaadhimishwa  kwa mara ya 16, likiwa na  mada inayosema “miaka 50 ya mchango wa wahandisi  kwenye Taifa, mafanikio, changamoto na mikakati ya baadae, ambapo kongamano hilo litarajiwa kumalizika keshokutwa, huku ikihusisha majadiliano na mada kutoka kwa watu mbalimbali.

Katika maadhimisho hayo ya siku tatu yanatarajiwa kuhudhuriwa na  viongozi mbalimbali wa Serikali, mashirika ya umma, na binafsi, na wageni kutoka nchi za Zambia, Nigeria, Ghana, Uganda, Ethiopia, Rwanda, Misri, Malawi na Kenya.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi