Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bodi ya Filamu Yamaliza Mzozo Malipo Filamu ya Utu Wangu
Jan 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28161" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo akipitia nyaraka za makubaliano ya mauziano ya Filamu ya Utu Wangu baina ya Mtayarishaji wa Filamu hiyo Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) na Kampuni ya Steps Entertainment wakati wa kikao cha usuluhishi leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu kufuatia mlalamikaji ambaye ni mtayarishaji wa filamu hiyo kufikisha malalamiko ya kutolipwa haki yake tangu mwaka 2015.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Hatimaye Bodi ya Filamu nchini imerejesha furaha kwa msanii na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu kufuatia kuongoza kikao cha usuluhishi kilichofikia muafaka  kwa msanii huyo kulipwa stahiki zake.

Hayo yamejitokeza leo wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya Msanii  Sikujua Mbwembe mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment  kilichofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

[caption id="attachment_28162" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kikao cha usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa Filamu ya Mtu Wangu, Bw. Andrew Makungu ambaye pia ni mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu akielezea jambo mbele ya wajumbe wa kikao hicho kilichohudhuriwa na uongozi wa Kampuni ya Steps Entertainment pamoja na upande wa mdai ambaye ni Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.[/caption] [caption id="attachment_28163" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Spets Entertainment Dilesh Solanki akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kikao cha usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Madai hayo yanahusi kutolipwa kwa haki za mauziano ya filamu hiyo waliyokubaliana tangu mwaka 2015, hata hivyo suala hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya Steps kuamua kulipa deni hilo. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Steps ambaye ni mtumishi wa zamani wa Cosota Bw. Yustus Mkinga na kulia ni Mtayarishaji wa Filamu John Lister.[/caption]

“Nitumie fursa hii kumshukuru Dilesh Mkurugenzi wa Steps kwa kukubali wito lakini pia kukiri kuwa msanii huyu haja;ipwa stahiki zake na kuamua kumaliza suala hili kwa kumlipa kwa jasho lake Bibi. Sikujua” alisema Mama Fissoo.

Mama Fissoo ameishukuru Kampuni ya Steps kwa hatua ilizochukua na kusema kuwa huo ni muendelezo way ale ambayo walikubaliana huko awali ikiwemo kuwalipa wale wote wanaoidai Kampuni hiyo jambo ambalo wameanza kulitekeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Steps Entertainment Dilesh Solanki amesema kuwa wao kama kampuni inayojihusisha na mambo mbalimbali ikiwemo usambazaji wa filamu hawafurahishi na kuona wana ingia migogoro na wasanii kwa hao ndio wateja wao muhimu.

[caption id="attachment_28164" align="aligncenter" width="750"] : Mwanasheria wa Kampuni ya Spets Entertainment inayojishughulisha na usambazaji wa Filamu Bw. Yustus Mkinga akifafanua jambo wakati wa kikao cha usuluhishi usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Mwaka 2015 Kampuni ya Steps iliingia mkataba wa kumiliki filamu hiyo kwa makubaliano ya kulipa sh. 7.5 milioni ambazo mpaka leo hawajalipa hali iliyopelekea madai hayo kufikishwa katika Ofisi za Bodi ya Filamu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Kutoka kulia ni Watayarishaji wa Filamu Suleiman Omary (Suleshi) na John Lister, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainments Dilesh Solanki.[/caption] [caption id="attachment_28165" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainments Dilesh Solanki (katikati) akisikiliza kwa makini hoja iliyokuwa ikitolewa na Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) wakati wa kikao cha usuluhishi usuluhishi wa madai ya msanii wa filamu na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembe leo jijini Dar es Salaam. Mwaka 2015 Kampuni ya Steps iliingia mkataba wa kumiliki filamu ya Utu Wangu iliyotayarishwa na msanii Sikujua Mbwembe (hayupo pichani) na kuingia makubaliano na Septs ya kulipwa sh. 7.5 milioni ambazo mpaka leo hawajalipa hali iliyopelekea madai hayo kufikishwa katika Ofisi za Bodi ya Filamu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Kutoka kulia ni John Lister na Mwanasheria wa Kampuni ya Spets Entertainment Yustus Mkinga.[/caption] [caption id="attachment_28166" align="aligncenter" width="590"] Mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu Bi. Sikujua Mbwembwe akiwa ndani ya Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (hayupo pichani) alipohudhuria kikao cha usuluhishi wa madai yake dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_28167" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Dilesh Solanki akibadilishani mihutasari ya kikao cha usuluhi wa madai ya msanii wa filamu Bi. Sikujua Mbwembwe ambaye aliilalamikia Steps kutomlipa stahiki yake kufuatia kuwauzia kazi yake ya filamu ya Utu Wangu mara baada ya kumaliza kikao na kufikia muafaka wa Steps kumlipa msanii huyo pesa zake kuanzia tarehe 5 Februari 2018. Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo. (Na: Mpiga Picha Wetu)[/caption]

Aidha amesema kuwa shida ambayo ilipelekea kutoka kwa tatizo la malipo kwa msanii huyo ni kitendo cha kuwepo kwa mtu wa kati ambaye kwa kiasi kikubwa bndiye amekuwa akifanya mawasiliano nao tofauti na mhusika mkuu.

“Tunakiri kuwa kuna namna ambavyo uzembe ulifanyika, sisi kama Steps tunabeba jukumu la kumlipa msanii huyu, jambo lingine niseme tu tumekwisha tekeleza makubaliano ya mazungumzo yetu, wasanii karibia wote waliokuwa wanadai tumewalipa wamebaki kama wanne tu hivi” alisema Dileshi.

Kwa upande wake Msanii Sikujua Mbwembwe ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kusema kuwa ameamini kweli kwamba Awamu ya Tani ni Serikali ya kutetea wanyonge ndiyo maana leo hii haki yake anaenda kuipata kwani ameangahika kwa muda mrefu sana.

“Binafsi nipende kuchukua fursa hii kuishukuru sana Serikali kupitia Ofisi yetu ya Bodi ya Filamu Tanzania, nimeleta malalamiko yangu tumekaa vikao vitatu haki yangu imepatikana keli Mungu ni mwema sana” alisema Bi. Sikujua.

Sikujua Mbwembe ni msaani mwenye ulemavu wa miguu ambaye alitayarisha filamu yake ya Utu Wangu na kuingia mkataba na Kampuni ya Steps Entertainment na kukutana na misukosuko katika malipo yake hata hivyo hii inaonyesha alipita katika njia zisizo sahihi, pamoja na yote hayo baada ya kuwasilisha madai yake katika mamlaka husika suala lake limeshughulikiwa na sasa anataraji kulipwa fedha zake na kunufaika na jasho lake mwenyewe.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi