Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bodi Mpya ya TAWA Yaaswa Kusimamia Sheria
Apr 18, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_42276" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akisisitiza jambo mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) pamoja na Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii leo Jijini Dodoma.[/caption]

Na Frank   Mvungi

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala ameitaka Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kusimamia kikamilifu Sheria na Taratibu zote ili kuhakikisha matokeo tarajiwa yanafikiwa kwa wakati.

Akizungumza wakati akizindua Bodi ya Mamlaka hiyo Waziri Kigwangala amesema kuwa, dhamira ya Serikali ni kuona TAWA inajiendesha kibiashara na kuongeza kiwango cha gawio kwa Serikali kutokana na kuongezeka kwa mapato.

[caption id="attachment_42277" align="aligncenter" width="900"] . Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_42278" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akieleza umuhimu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii leo Jijini Dodoma.[/caption]

“Jukumu lenu kama Bodi ni moja tu la kuhakikisha kuwa mnasimamia sheria kanuni na taratibu zilizopo na kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kurudisha nyuma maendeleo ya sekta hii na hivyo kushindwa kutoa mchango mkubwa katika pato la Taifa.” Alisisitiza Dkt Kigwangala.

Akifafanua  amesema  kuwa, Bodi hiyo inapaswa kufanya kazi kwa kasi inayoendana na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano hivyo wajumbe wote wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa wakati na kwa kuzingatia tija na malengo ya Taifa.

 Akizungumzia sekta ya wanyamapori kwa ujumla, Waziri Kigwangala amesema kuwa sekta hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo ni wakati sasa kwa Bodi hiyo mpya kufanya mageuzi kwa kutatua changamoto kwa wakati na kusimamia kikamilifu uendelezaji wa sekta hiyo muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

[caption id="attachment_42279" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Leo Jijini Dodoma mara baada ya kuzindua Bodi hiyo pamoja na Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii.[/caption] [caption id="attachment_42280" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala (katikakati) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko (kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii Dkt. David Manyanza[/caption]

“Sekta hii ni muhimu kwa wananchi na kichocheo cha ustawi wa sekta nyingine ambazo zina mchango katika kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini hivyo ni muhimu kusimamia sekta hii kwa kuzingatia sheria , kanuni na taratibu” Alisisitiza Dkt. Kigwangala

Akieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimrisha utendaji wa TAWA amesema kuwa ni pamoja na kuundwa kwa Bodi mpya yenye wajumbe wenye sifa na weledi unaohitajika katika nyakati hizi ili kukuza sekta ya wanyamapori nchini.

[caption id="attachment_42281" align="aligncenter" width="900"] Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt. Allan Kijazi akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala mara baada ya kuzindua Bodi ya Mamlaka hiyo leo Jijini Dodoma pamoja na Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii.[/caption] [caption id="attachment_42282" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. Dkt. James Wakibara akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Bodi ya Mamlaka hiyo leo Jijini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO)[/caption]

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis   Semfuko amesema kuwa Bodi hiyo itatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Aliongeza kuwa  watahakikisha mchango wa TAWA katika kukuza pato la Taifa unaongezeka kufikia asilimia 35 hali itakayosaidia katika kuchochea maendeleo ya sekta hiyo na Taifa kwa ujumla.

Uzinduzi wa Bodi ya TAWA umefanyika Jijini Dodoma Aprili 17, 2019 ukilenga kuchochea maendeleo na kukuza sekta hiyo.Uzinduzi wa Bodi hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi