Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 6.1 Zagharamia Miradi ya Kijamii Vijiji Vinavyopakana na Misitu
Aug 16, 2023
Bilioni 6.1 Zagharamia Miradi ya Kijamii Vijiji Vinavyopakana na Misitu
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kuelezea utekelezaji na mafanikio ya TFS kwa mwaka wa fedha 2022/23 na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO

Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa kipindi cha 2022/2023 umetoa misaada mbalimbali yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 6.1 kwa kugharimia miradi mbalimbali ya jamii katika vijiji vinavyopakana na hifadhi za misitu.

Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo ameyaeleza hayo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji na mafanikio ya wakala hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/23 na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Prof. Silayo anasema kuwa, miradi hiyo imeimarisha huduma vijijini kwa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, maji, afya, biashara na masoko, ukarabati barabara za vijiji, michezo, mashamba kwa ajili kilimo mseto, misaada kwa jamii yenye mahitaji maalum, utawala bora na ujenzi wa vituo vya Polisi au ofisi za vijiji.

Aidha amebainisha kuwa, TFS ilishiriki vyema katika miradi mbalimbali ya kimakati ya taifa, ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni mkatati wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani na kusafisha eneo la mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

“TFS iliingia makubaliano ya kimkakati na Jiji la Dodoma kuainisha maeneo makuu ya mashirikiano, lengo la kutekeleza mpango wa ‘Dodoma ya Kijani’ ni kuzuia mmomonyoko wa udongo, uharibifu wa mazingira na kuongeza uoto wa asili katika jiji la dodoma na vitongoji vyake,” ameongeza Prof. Silayo.

Malengo mengine ni pamoja na kulifanya jiji hilo na maeneo ya jirani kuwa na uoto utakaopendezesha mandhari na kuweka mazingira stahimilivu na yenye afya ya kuwezesha maisha ya wakaazi wake kuwa bora zaidi ambapo katika kipindi cha mwaka jana jumla ya miche 1,228,200 imepandwa sawa na eneo la hekta 3,075.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi