Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Benki ya Kilimo Yatinga Hong Kong Kutafuta Fursa za Uwekezaji
Nov 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21582" align="aligncenter" width="756"] Pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Francis Assenga mara baada ya kupitia Mchoro wa Ramani ya Mkakati wa Kiuchumi wa 'One Belt One Road' mjini Hong Kong hivi karibuni kwenye tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo kupitia Mkakati huo.[/caption] [caption id="attachment_21583" align="aligncenter" width="1008"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzainia (TADB) Bw.Francis Assenga (Katikati) akiwa na viongozi mbali mbali mara baada ya kumalizika kwa Kikao chake na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa China Capital Fund Management (Hong Kong) Bw. James Wang (kushoto kwake). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa First Shanghai Capital Ltd Bwana Allen Wang, Mkurugenzi wa Landmark Investments Hong Kong na Mjumbe wa Kudumu wa Kamati ya Bunge la China Dr. Annie Wu Chung, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kuhamasisha Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bw. Joseph Kahama na Mkurugenzi Mtendaji wa First Shanghai Capital Ltd Bi. Fanny Lee.[/caption] [caption id="attachment_21584" align="aligncenter" width="1008"] Kikao kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya kutafuta mitaji na uwekezaji ya Hong Kong iitwayo China Alpha Fund Management (HK) kilichofanyika katika Jengo la Two Exchange Square mjini Hong Kong hivi karibuni ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Utafutaji Mitaji na Uwekezaji ya Hong Kong Bwana James Wang (Katikati). TADB iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bwana Francis Assenga (Mwenye Shati la Bluu na Tai) na kushoto kwake ni Bwana Joseph Kahama ambaye ni Katibu Mkuu wa China-Tanzania Friendship Promotion Association. Kushoto wa Kwanza ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Wawekezaji wa China Alpha Fund Management (HK) Ltd Bi. Kandice Au.[/caption] [caption id="attachment_21585" align="aligncenter" width="1008"] Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Francis Assenga mwenye tai nyekundu kulia kabisa akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya China Hong Kong baada ya kumalizika kwa Kikao chao mnamo tarehe 20 Oktoba 2017. Kulia kwa Bw. Assenga ni Meneja Mkuu wa BOC Hong Kong Bwana Chan Man Stephen, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Ushirikiano kati ya China na Tanzania Bwana Joseph Kahama na Watendaji wa Benki hiyo Bi. Yiu Oi Yin Doris, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Biashara inayoshughulikia Taasisi za Fedha na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa Mahusiano na Mabenki, Bw.Wong Chee Him Steve wakiwa Makao Makuu ya Benki ya China mjini Hong Kong.[/caption] [caption id="attachment_21586" align="aligncenter" width="1008"] Bw. Francis Assenga katikati mwenye suti ya khaki ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB akipanda miti katika Shule ya Sekondari ya China Foundation mjini Hong Kong kuashiria kuunga mkono Mapinduzi ya Mkanda wa Kijani (Green Belt Revolution) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 35 ya shule hiyo ambapo Bw. Assenga alialikwa kama Mgeni Maalum wa Shule hiyo. Wageni wengine Maalum waliotoka nchi mbali mbali ni pamoja na Bw.Joseph Kahama ambaye alialikwa kama sehemu ya Jopo la Washauri wa Shule hiyo kwa miaka takriban nane sasa na Mkurugenzi Mtendaji wa Japan International Cooperation Foundation Bw. Takashi Kawasaki (Mwenye Suti bila Tai Kulia kabisa) toka Tokyo, Japan na Mkurugenzi wa China Mfuko wa Uhifadhi Mazingira na Maendeleo ya Mkanda wa Kijani Prof. Frederick Charles Dubee (Mwenye Mvi na Tai katikati) toka Hienola, Finland.[/caption] [caption id="attachment_21587" align="aligncenter" width="756"] Kaimu Mkurigenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary School (CFSS) Bw. Au Kwong Wing, zawadi toka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati Bw. Assenga alipokaribishwa kama Mgeni Maalum wa Shule kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Sekondari hiyo Mjini Hong Kong hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliwahimiza wanafunzi wa shule hiyo kuhifadhi mazingira na kujikita kwenye teknolojia mbali mbali za kilimo cha kisasa.[/caption] [caption id="attachment_21588" align="aligncenter" width="1008"] Baadhi ya Wageni Maalum toka nchi mbali mbali duniani walioalikwa kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya China Foundation Secondary School (CFSS) yaliyofanyika shuleni hapo nchini Hong Kong hivi karibuni. Wa Nne toka kushoto mwenye tai nyekundu ni Bwana Francis Assenga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).[/caption] [caption id="attachment_21589" align="aligncenter" width="750"] Wawakilishi wa Tanzania Bwana Francis Assenga (Kaimu Mkuruvenzi Mtendaji wa TADB) wa pili toka kushoto na Bwana Joseph Kahama (Katibu Mkuu wa Taasisi ya China-Tanzania Friendship Association) wakikabidhiwa Zawadi ya Utambuzi wa mchango wao kwenye shughuli za kiuchumi, kilimo na huduma za jamii kwenye Maadhimisho ya Miaka 35 ya Shule ya Sekondari ya Jiji Hong Kong. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bwana Au Kwong Wing na Kukia kabisa ni Mratibu wa Maadhimisho hayo (Mwene shati jeupe).[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi