[caption id="attachment_27493" align="aligncenter" width="815"] Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza umuhimu wa Kutunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhifadhi wa rasilimali maji awamu ya pili wa Wami- Ruvu Basin utakaotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia uliofanyika mapema leo Mjini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.[/caption]
Na. Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Benki ya Dunia imetoa ufadhili wa shilingi Bilioni 47 kutekeleza mradi wa uhifadhi wa rasilimali za maji awamu ya pili katika bonde la mto Wami.
Akizindua mradi huo mapema leo, Mjini Dodoma Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa Tanzania ina jumla ya mabonde tisa ya maji lakini mabonde hayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu na kiuchumi zinazosababisha kupungua kwa maji katika mabonde hayo.
[caption id="attachment_27494" align="aligncenter" width="750"]"Fedha hizi zilizotolewa na Benki ya Dunia zitaenda kutoa elimu kuanzia ngazi ya juu mpaka mwananchi wa kawaida juu ya njia za kutumika kutunza rasimalimali za maji ndani ya hifadhi ya bonde la mto Wami," alisema Mhandisi Kamwelwe.
Aidha Mhandisi Kamwelwe amewataka wananchi na viongozi watakaopata elimu hiyo kutunza rasilimali hiyo wao wenyewe kwa kutofanya shughuli za kibinadamu na za kiuchumi ndani ya hifadhi la bonde hilo.
[caption id="attachment_27496" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wake, mwakilishi wa Benki ya Dunia Alex William amesema kuwa jukumu la utunzaji wa rasilimali za maji ni za kila mwananchi, kiongozi pamoja na taasisi za umma na binafsiHivyo amewata Watanzania kupitia mradi huo kutunza rasilimali hiyo ili kuongeza kiwango cha maji ndani ya bonde hilo ambayo yatatumika katika shughuli za nyumbani, viwandani, mashambani katika shughuli za uvuvi pamoja na utalii.