Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bashungwa Atangaza Ukomo wa Bei za Barakoa, Aelekeza Viwanda vya Nguo Nchini Kutengeneza Barakoa
Apr 27, 2020
Na Msemaji Mkuu

 

[caption id="attachment_52310" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe. Innocent Bashungwa akitolea ufafanuzi wa bei ya barakoa ambapo ameagiza bei isizizi 1500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.[/caption]

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amesema atachukua hatua kwa Taasisi Zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazouza barakoa kwa gharama kubwa.

 

Bashungwa alitoa tahadhari hiyo mkoani Arusha alipotembelea viwanda vya kuzalisha nguo vya Sunflug na A to Z kuangalia hali ya uzalishaji wa barakoa katika viwanda hivyo.

 

Bashungwa alitoa onyo kwa NGOs zilizoomba kibali cha kuzalisha barakoa kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania lakini badala yake wanauza barakoa kwa shillingi 2,500 hadi 3,000.

 

“Wamekuwa wakitoa masharti kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawauzi barakoa chini ya bei hiyo, sitawataja kwa leo lakini nikiona tu wanauza kwa bei kubwa sitasita kuwachukulia hatua, maana mnakuja kuomba vibali kumbe mnafanya mtaji”, alisema Bashungwa.

 

Alisisitiza kuwa barakoa zote ziuzwe kwa bei isiyozidi 1500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.

 

Kwa upande mwingine Mhe. Bashungwa alivipongeza viwanda vya nguo vya A-Z na Sunflug kwa kuzalisha barakoa ambazo zinawasaidia watanzania walio wengi, na amewahaidi Serikali kuwapati ushirikiano.

 

Aidha alivitaka viwanda hivyo kuendelea kuzalisha kwa wingi ili wananchi walio wengi wa vijijini waweze kupata vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa korona.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo aliwataka wananchi wote wa mkoa huo kuchukua tahadhali zinazotolewa na Wizara ya Afya wanapotembelea maeneo yenye mkusanyiko.

 

Pia, alisisitiza kuwa ni vema sasa wafanyabiashara hao wakatengeneza barakoa kwa bei nafuu ili kuwezesha wananchi kununua.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi