Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Laaswa Kuongeza Ushiriki wa Sekta Binfasi
Oct 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36957" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akifungua mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi uliofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, ameongoza mkutano wa majadiliano ya Baraza la Biashara la mkoa huo ili kupitia na kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili usaidie kukuza ushiriki wa sekta binafsi na kuchochea ukuaji wa sekta zinatoa ajira kwa wananchi walio wengi kama kilimo.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo  leo Jijini Dodoma  na wadau wengine, Dkt. Mahenge amesema kuwa, mkutano huu una lengo la kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ngazi ya Mikoa na Wilaya.

“Tunategemea utakuwa rejea thabiti kwa viongozi na watendaji ambao wamekuwa wakibadilika mara kwa mara kutokana na uteuzi au chaguzi”. Alisisitiza Dkt. Mahenge

[caption id="attachment_36958" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith akiteta jambo na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa huo anayeshughulikia Sekta za Uchumi na Uzalishaji Bi Aziza Mumba mara baada ya mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi katika mkoa huo.[/caption]

Akifafanua zaidi, mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amesema mkutano huo wa majadiliano una lengo la kuhakikisha ushiriki wa sekta binafsi unaongozeka ili kuchochea maendeleo ya mkoa na taifa.

Aliongeza kuwa, majadiliano hayo yatasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza mara kwa mara ambazo zimekuwa zikifubaza upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kijamii na yanategemewa kutoa ufumbuzi wa changamoto  hizo kwa kuzingatia maandalizi ya majadiliano, kanuni za majadiliano na utekelezaji baada ya majadiliano.

“Ninatambua kuwa Mabaraza ya biashara yapo katika Wilaya zote mkoani hapa hivyo naamini yatatumika ipasavyo  na yatawezesha kuchochea Maendeleo katika Mkoa na Wilaya zetu kwa kushawishi ongezeko la biashara na uwekezaji”. Alibainisha Dkt. Mahenge.

[caption id="attachment_36959" align="aligncenter" width="900"] Mhadhiri kutoka Chuo kikuu Mzumbe Prof. Honest Ngowi akiwasilisha rasimu ya mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi wakati wa kikao cha kujadili muongozo huo leo Jijini Dodoma.[/caption]

Pia aliwahimiza  viongozi wa kisiasa na watendaji wote wahakikishe mabaraza ya biashara yanakuwa hai katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

Aidha, aliwataka viongozi katika ngazi za Wilaya kuboresha mazingira ya biashara yatakayowezesha wananchi  kutoa mchango kwenye pato la mkoa na taifa kwa ujumla.

Michango ya wadau itakuwa imejumuishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa 10. Baada ya Mwongozo kukamilika utazinduliwa rasmi na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa tarehe itakayopangwa.

[caption id="attachment_36960" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya wakuu wa Wilaya wa mkoa wa Dodoma wakifuatilia mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi uliofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_36956" align="aligncenter" width="900"]
 Sehemu ya washiriki mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi uliofanyika leo Jijini Dodoma.
                                                                                                              (Picha zote na MAELEZO)[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi