Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri waaswa kutumia mifumo ya Usimamizi wa fedha za Umma ili kuleta Tija
Jun 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

Afisa usimamizi wa fedha kutoka TAMISEMI Bw.Elisa Rwamiago akifungua mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro leo Mkoani Iringa.

Wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri  wameaswa kutumia mifumo  iliyofungwa kwenye halmashauri zao ili kuleta ufanisi wa utendaji kazi.

Hayo yamesemwa leo na Afisa usimamizi wa fedha kutoka TAMISEMI Bw.Elisa Rwamiago wakati  akifungua mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) leo mkoani Iringa.

“Mafunzo haya ya mfumo wa Epicor toleo la 10.2 ni moja ya maboresho yanayoendelea kufanywa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo ambao ni Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) hivyo ni muhimu kuitumia kwa ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa letu.

Afisa usimamizi wa fedha kutoka TAMISEMI Bw.Elisa Rwamiago akifungua mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro leo Mkoani Iringa.Kulia kwake ni Mtaalamu Mshauri wa masuala ya rasiliamali fedha kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi Hellen Nyagwa na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Iringa Bw.Baraka Mwambene.

Aidha Afisa uyo amesema kuwa lengo la maboresho ya mifumo hiyo ni kuhakikisha usimamizi katika serikali za mitaa unaimarika pia kumwezesha mhasibu au mweka hazina kufanya kazi zake kwa urahisi zaidi.

Ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi katika kutumia mifumo mbalimbali iliyokuwa ikitumika kipindi cha nyuma  na ndio  maana kuwekuwa na maboresha kila mara ya mifumo hii katika halmashauri.

Pamoja na hayo amesema kuwa maboresho ya mifumo hii yanaweza kuboresha utendaji wa mtu binafsi lakini kama hayatasimamiwa ipasavyo yataweeza kumuingiza muhasibu katika matatizo makubwa.

“Inapoanzishwa mifumo hii ni vyema tukajiwekea vipaumbele vya kufanya,jukumu lenu la kwanza ni usimamizi wa fedha na hivyo hakuna mtu atasimamia vyema fedha za umma kama hajajifunza mifumo hii mipya inayotakiwa kutumika,ni muhimu mjifunze mifumo hii ili muweze kuwajibika katika maeneo yenu,tubadilike kuendana na matakwa ya mifumo,Aliongeza Bw.Rwamiago.

Mtaalamu Mshauri wa masuala ya rasiliamali fedha kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi Hellen Nyagwa akielezea ufanyaji kazi wa  Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro leo Mkoani Iringa.Kulia kwake ni Afisa usimamizi wa fedha kutoka TAMISEMI Bw.Elisa Rwamiago

Wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) leo Mkoani Iringa.

Aidha amewataka wahasibu na weka hazina hao kupunguza changamoto zinazotokana na uzembe au usimamizi duni wa mifumo hii na kusimamia mifumo hii kwa uangalizi wa hali ya juu.

Aidha ametoa shukurani za pekee kwa wafadhili wa  Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Kwa upande wake Mtaalamu Mshauri wa masuala ya rasiliamali fedha kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Bi Hellen Nyagwa amesema kuwa mfumo huu wa epicor 10.2 utaleta mabadiliko makubwa katika utumishi wa umma na hivyo kuwaasa washiriki hao kujifunza na kuulewa vyema ili kuleta tija katika nchi.

Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni Mradi wa miaka mitano unaotekelezwa katika mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara.  PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.

Wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) leo Mkoani Iringa.

Wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) leo Mkoani Iringa.

Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI  Bw.Juma Shaha akielezea umuhimu wa matumizi ya mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro leo Mkoani Iringa.

Wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) leo Mkoani Iringa.

Mhasibu kutoka Mkoa wa Songwe Bw.David Johnson akifafanua jambo kwa washiriki wa mfumo wa Usimamizi wa fedha za Umma toleo la 10.2 (Epicor 10.2) kwa wahasibu na Waweka hazina wa Halmashauri za Iringa, Tanga,Morogoro na Kilimanjaro leo Mkoani Iringa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi