Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Asali ya Tanzania Yazidi Kupata Soko
Jul 03, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_5221" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Mhandisi Christopher Chiza (wakwanza kushoto) akionja asali inayozalishwa Tanzania wakati wa siku ya asali iliyoadhimishwa leo ikiwa ni sehemu ya maonesho ya Kimataifa ya 41 biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere ,barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE Bw. Edwin Rutageruka.[/caption]

Na. Frank Mvungi

Wazalishaji wa asali nchini wametakiwa kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi ambalo limeendelea kukua na kuchochea maendeleo ya sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekitiwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Mhandisi Christopher Chizawa wakati akifungua maonesho ya siku ya asali yaliyoafanyika leo katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Maonesho ya Kimataifaya Dar es Salaam (Sabasaba).

“Kila mwaka tunapeleka asali nje ya nchi hasa Ujerumani na hatujawahi kupata malalamiko kutoka huko ambako kuna maabaraza kisasa za kupima ubora wa asali na matokeo yamekuwa yakionyesha asali yetu ina ubora unaotakiwa hali inayochochea mahitaji ya asali kutoka Tanzania kwenda Ulaya na sehemu mbalimbali kuwa makubwa”, alisisitiza Mhe. Chiza

Mwenyekiti wa Bodi alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwaTaasisi zote zinazo husika na sekta ya asali na mazao ya misitu zinasimamiwa vyema ili ziendelee kutoa matokeo chanya yatakayo changia katika kukuza uchumi wan chi na kuwakwamua wazalishaji wa asali.

Pia aliwataka wazalishaji wa asali kuweka mkazo katika kuongeza uzalishaji unaendana na mahitaji ya soko la Kimataifa kwa kuwa mahitaji ya asali toka Tanzania ni mkubwa hali inayo toa chanagamoto kwa wazalishaji kuongeza kasi ya uzalishaji huku wakizingatia ubora unaotakiwa katika soko.

[caption id="attachment_5222" align="aligncenter" width="750"] Msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya Central Park Bees Bi Sophia Chilambo akionesha moja ya mizinga ya kisasa inayotumika katika ufugaji wa nyuki wakati wa siku ya asali.[/caption]

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Zawadi Mbwambo amesema kuwa wakala huo unaendelea kusimamia sekta hiyo ili kuhakikisha kuwa inakuwa salama na inatoa matokeo tarajiwa katika uchumi hasa kuchochea ujenzi wa viwanda vya kusindika asali hapa nchini.

Aliongeza kuwa ufugaji wa nyuki una gharama nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kumudu katika mazingira yake na hivyo kukuza kipato chake na kuchangia katika kuchochea maendeleo kwa kuzalisha ajira na kuongeza fedha za kigeni hapa nchini.

[caption id="attachment_5223" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wananchi waliofika katika banda la asali wakitazama asali inayozalishwa na wajasiriamali wa Tanzania.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)[/caption]

Kwa upande wake mmoja wa wajasiriamali wanaozalisha asali kutokaKikundi cha mama wawili product amesema wanaipongeza Serikali kwa juhudi inazochukua katika kuwainua wajasirimali wanaozalisha asali hapa nchini kwa kuwawezesha kushiriki maonesho ya 41 Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kuongeza kuwa asali ya Tanzania inakubalika kimataifa kwa ubora wake hivyo changamoto iliyopo ni kuongeza uzalishaji.

Siku ya asali Iimeadhimishwa leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Maonesho ya Kimataifa ya Biasharaya Dar es Salaam yaliyoanza June 28 hadi Julai 13 mwaka huu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoa agizo katika halfa ya ufunguzi wa maonesho hayo kuwa muda wa maonesho uongezwe kwa siku tano zaidi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi