Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

AREPEB Kuendeleza Amani Nchini
Oct 06, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_17407" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB) Bi. Imelda Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa mfumo wa Kieletroniki wa ukuzaji amani, Haki za Binadamu na misingi ya utawala bora, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi katika mikutano Mikuu toka Shirika hilo Yohana Mcharo na kulia ni Katibu Mkuu wa shirika hilo Julius Muganga. (Picha na Eliphace Marwa)[/caption]

Na: Thobias Robert

Shirika lisilo la kiserikali la Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB)  limezindua mfumo wa kielektroniki wa ukuzaji amani, haki za binadamu na misingi ya utawala bora ili kufikia maendeleo ya Tanzania ya viwanda.

Uzinduzi huo umefanyika Jijini Dar es Salaam leo na viongozi wa Shirika hilo katika mkutano na waandishi wa Habari ambapo shirika limetoa namba za simu kwa lengo la kupata maoni, ushauri pamoja na mapendekezo ya kuendeleza amani hapa nchini kwa ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.

“AREPEB inachukua fursa hii kuzindua mfumo wa kielectroniki ukataotumika kukusanya maoni kuhusu ukuzaji amani nchini, taarifa kuhusu masuala ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa kutumia ujumbe wa maneno kupitia namba 0800712121 au +255757333773 (ujumbe wa maneno) na +255758333773 kwa ujumbe wa sauti na ujumbe hautakuwa na malipo,” alifafanua Bi. Angela Thadei Mwanansheria wa Shirika hilo.

Aliendelea kusema kuwa, mfumo huo ni huru kwa wananchi wote bila kujali, dini, itikadi za kisiasa, ukanda au ukabila, hivyo  ametoa wito kwa wanachi kuutumia mfumo huo vizuri ili kila mwananchi aweze kuchangia maoni yake ili kuimarisha amani nchini.

“Maoni, ushauri na malalamiko yote yatakayotolewa ama kukusanywa, yatafanyiwa kazi na kupata taarifa muhimu ambayo itatumika kushauri mamlaka husika, ili kuchukua hatua kufikia matakwa ya wananchi walio wengi kuhusu kuheshimu amani tuliyonayo, haki za binadamu na misingi ya utawala bora,” alisisitiza Bi. Thadei.

Aidha, kupitia ufadhili wa Foundation for Civil Society, AREPEB inatekeleza mradi wa amani (Peace Programe), haki za binadamu na utawala bora ambao utafanyika kwa awamu kipindi cha miezi sita kati ya mwezi  Agosti hadi Oktoba 2017 na mwaka 2018, kuanzia mwezi Februari hadi Machi.

“AREPEB inatambua umuhimu wa kutumia vyombo vya habari kusanmbaza taarifa nchini na na kuwa ni wadau wakubwa katika ukuzaji na ujenzi wa amani, haki za binadamu na misingi ya utawala bora, hivyo inachukua fursa hii adimu kuviomba vyombo hivyo kushiriki kuelimisha umma kuhusiana na program hii,” alieleza Bi. Thadei.

Aidha program inayohusisha mafunzo ya amani na utatuzi wa migogoro pamoja na haki za binadamu na misingi ya utawala bora inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Pwani (Kibaha) kuanzia tarehe 7 na 8 mwezi huu.

Aidha kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi katika Mkutano Mkuu wa Shirika hilo Bw, Yohana Mcharo alitoa wito kwa vyombo vya usalama kuendelea kulinda amani ya Wananchi na rasilimali zao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu, lakini pia kila mmoja kwa nafasi yake analo jukumu  la kuilinda amani na utulivu vyilivyodumu kwa muda hapa nchini.

Shirika hili la AREPEB lilianzishwa na kusajiliwa na Serikalini mwaka 2014, kwa lengo la kushughulikia masuala ya ukuzaji wa amani, haki za binadamu na misingi ya haki za binadamu, utoaji wa elimu kwa umma, usuluhishi wa migogoro na kutoa mijadala ya amani hapa nchini.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi