[caption id="attachment_9689" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Uthibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Lazaro Kitandu akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waandisi wa Habari kuhusu mfumo mpya wa uagizaji wa mbole kwa pamoja leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Issa Sabuni.[/caption]
Na: Paschal Dotto
Wakulima wanatarajia kupata mbolea kwa bei nafuu tofauti na hapo zamani ambapo hivi sasa Serikali imekuja na mfumo mpya wa uagizaji wa mbolea kwa wakulima wote katika maeneo yote Tanzania hususani maeneo ya vijijini ambako mbolea ilikuwa inafika kwa gharama kubwa.
Akizungumuza Jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania(TFRA) Bw. Lazaro Kitandu amesema kuwa huduma ya upatikanaji wa mbolea kwa wakulima wote nchini utarahisishwa kwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo imeweka utaratibu mpya wa uagizaji wa mbolea kwa kutoa tenda kwa wazabuni mbalimbali.
[caption id="attachment_9691" align="aligncenter" width="750"]“Serikali imechukua hatua ya kuanzisha utaratbu mpya wa kuagiza mbolea kwa pamoja kutoka zinakotengenezwa, yaani mbolea za kupandia (DAP) na mbolea za kukuzia(UREA) kupitia kwa wawekezaji wanaochukua zabuni hiyo”,alisema Kitandu.
Hatua nyingine ambazo serikali imechukua katika kuboresha sekta ya kilimo ni pamoja na Mamlaka hiyo kuweka matarajio ya matumizi makubwa ya mbolea ili kuendana na kasi ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Tanzania ina matumizi ya asilimia 19 ya mbolea kwa hekta moja ambayo ni matumizi madogo,nchi nyingine zina matumizi ya asilimia 50 kwa hekta moja kwa hiyo mamlaka inaweka matarajio makubwa kwa matumizi ya mbolea ili kuinua kilimo na kujenga uchumi wa viwanda.
[caption id="attachment_9692" align="aligncenter" width="750"]Aidha Bw. Kitandu alisema mchakato wa kumpata mzabuni wa kazi hiyo ya uagizaji mbolea ulianza mwezi Aprili kwa kutangaza zabuni kwa makampuni mbalimbali ambapo kufikia mwezi Julai, 2017 washindi walipatikana ambao ni kampuni ya OCP ya Morocco na Premium Agrocam ya Tanzania.
“kufuatia utaratibu huu mpya mchakato ulianza tangu mwezi aprili kwa kuchuja watu ambao wanauwezo wa kutuleta mbolea ,lakini mchakato uliendelea mwezi Julai tukapata mzabuni wa mbolea za kupandia(DAP) ambapo Kampuni ya OCP kutoka Morocco ilibuka washindi katika zabuni hiyo na kumpuni ya Premium Agrocam kuwa mzabuni wa mbolea ya kukuzia yaani (UREA)”, alisema Bw. Kitandu.
Bw.Kitandu alivitaja vigezo vilivyotumika kumpata mzabuni huyo kuwa ni pamoja na bei inayopatikana katika viwanda vinavyotengeneza mbolea ambapo OCP pamoja na premium agrocam walionekana kuwa na bei za kuridhisha.
[caption id="attachment_9697" align="aligncenter" width="750"]Aidha Bw. Kitandu aliwahakikishia wakulima kuwa mbolea itasafirishwa mpaka vijijini kwa kutumia treni na malori kwa sehemu ambapo treni haiwezi kufika, na amewatoa hofu wakulima kuwa msimu unaoanza mwezi wa tisa wameagiza tani 23,000 kwa mbolea ya kupandia (DAP) na tani 32,000 kwa mbolea ya kukuzia (UREA) ambapo watakuwa wanaagiza kwa awamu kwa miezi miwili miwili.
Tanzania inatumia Tani 4000,000 kwa mwaka na kwa kwa msimu huu bei ya mbolea itashuka kutoka aslimia 15 mpaka asilimia 40, ambapo kwa mfuko wa kilo 50 utanunuliwa kwa shilingi 52, 000 badala ya shilingi 1000,000 bei ya awali.
Pia amewaonya wale watakaotumia mwanya huu kuuza mbolea nje ya bei elekezi ya Serikali kwamba watachukuliwa hatua za kisheria kama kunyang’anywa leseni, kufungwa, faini au vyote kwa pamoja.