Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro akipata (aliyeshika kiuno) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesjheni za Jeshi la Polisi, DCP Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa kwa wahalifu 13 katika majibizano ya lisasi kati ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangi Bovu, kijiji cha Miwalewni tarafa ya Kibiti. Chini ni bunduki nane aina ya SMG na vifaa vingine vilivyopatikana.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro akiangalia vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika majibizano ya lisasi kati ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangi Bovu, kijiji cha Miwalewni tarafa ya Kibiti ambapo bunduki nane aina ya SMG, risasi 158, pikipiki mbili pamoja na begi la nguo vilikuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kulia ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz.
(Picha Zote na Jeshi la Polisi)